INEC YAVITAKA VYAMA VYA SIASA KUTOINGILIA MCHAKATO UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA

 


📌RHODA SIMBA

TUME huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewasisitiza Mawakala na viongozi wa vyama vya siasa, kutokuingilia mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kituoni.

Hayo yamesemwa leo Septemba 13,2024 jijini Dodoma, na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mahakama ya Rufaa Mbarouk Salim Mbarouk, wakati akifungua Mkutano wa INEC kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Hivyo niwaombe viongozi wa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kwa ujumla kuzingatia sheria za uchaguzi, kanuni za uboreshaji, maelekezo ya Tume na kusimamia miiko na mipaka ya undeshaji wa zoezi la uboreshaji daftari,

Amesema kuwa ni vyema wakatumia sheria zilizopo kuwasilisha kwa Tume changamoto zitakazijitokeza, na kusema kuwa kwa upande wao watazingatia katiba, sheria ya uchaguzi na kanuni zilizotungwa chini ya sheria katika zoezi hilo la uboreshaji. 

Jaji Mbarouk amewahimiza wadau hao kupitia majukwaa yao ya kisiasa, kijamii, kitamaduni, kiimani na kiuchumi kuwakumbusha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. 

Ni mategemeo yetu kuwa michango na maoni watakayotoa kwenye mkutano huo yatakuwa na manufaa makubwa katika kutekeleza zoezi ambalo lipo mbele yetu,

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi Selemani Mtibora amesema, kwa Mkoa wa Dodoma kuna vituo 2,721 vitakavyotumika kwenye uboreshaji kwa nwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 37 katika vituo 2,684 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.

Mtibora ameongeza kuwa jumla ya wapiga kura 594,494 wanatarajiwa kushiriki zoezi hilo ambapo watakao kosa sifa wataondolewa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. 

Hivyo, baada ya uboreshaji inatarajiwa kuwa daftari litakuwa na jumla ya wapiga kura 34,746,638 pia idadi hii inaweza kuongezeka kwa kuwq inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa daftari la uboreshaji mwaka 2019/20 lakini kwasababu moja au nyingine hawakuweza kujiandikisha kuwa wapiga kura,

Naye Mratibu wa uandikishaji Mkoa wa Dodoma Charles Mduma amevielekeza vyama vya siasa kuzingatia mafunzo na maelekezo yanayotolewa na tume yanl uchaguzi ili kila mtu atimize wajibu wake.

Mafunzo haya ya leo tumepewa majukumu ya kwamba wanasiasa wanajukumu ganj katika zoezi hili la uboreshaji kwahiyo sana sana naendelea kuwaelekeza wafuate na kuzingatia yale yaliyofundishwa ili uchaguzi uweze kwenda vizuri,

                         



Post a Comment

0 Comments