BENKI ya NMB imepongezwa kwa
kuunga mkono jitihaada za serikali kwenye setka ya afya, kupitia utekelezaji wa
sera yake ya kutenga asilimia moja ya faida wanayopata na kurejesha kwenye
jamii CSI ambapo kwa mwaka huu pekee zaidi ya sh billion tano zimetengwa
kwaajili ya kazi hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Moduli Festo Kiswaga ameyasema hayo muda mfupi kabla ya kupokea msaada wa vifaa tiba kutoka benki ya NMB kwaajili ya hospitali ya wilaya ya Monduli vikiwemo vitanda vya kulalia wagonjwa na magodoro yake, mashuka ya kujifunika wagonjwa, stand za kutundikia drip za dawa za maji, pamoja na viti vya magurudumu matatu kwaajili ya kusukumia wagonjwa.
Mkuu wa Wilaya huyo wa Monduli amesema serikali ya awamu ya sita pamoja na mambo mengine imeelekeza nguvu zake katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za afya, elimu bora na utunzaji wa mazingira sekta ambazo ndizo kipaumbele cha benki ya NMB katika kurejesha sehemu ya faida wanayopata kwa jamii hivyo wamekuwa wakiunga mkono serikali kwa a silimia mia moja kwenye sekta hizo.
Kwa upande wao benki ya NMB kupitia Mkuu wa Idara ya huduma za Serikali Vicky Bishubo amesema ni sera ya benki ya NMB kutenga asilimia moja ya faida wanayopata baada ya kodi kwaajili ya kurudisha kwa jamii, wakizingatia faida na mafanikio makubwa ambayo benki inaendelea kupata yanatokana na jamii inayowazunguka, na katika kufanikisha hilo wamejikita zaidi kwenye sekta ya elimu, afya, mazingira na majanga pale yanapojitokeza.
Benki ya NMB imejiwekea sera ya kutenga asilimia moja ya faida wanayopata baada ya kodi kila mwaka na kurejesha kwa jamii inayowazunguka, ambapo kwa mwaka 2023 benki ilitengeneza faida ya Shilling billion 542 baada ya kodi na hivyo kwa mwaka huu pekee zaidi ya billion tano zimetengwa kwaajili ya kurudisha kwa jamii.
0 Comments