WAFUGAJI KUKU WASHAURIWA KUACHA MAZOEA

 


 ðŸ“ŒSAIDA ISSA

WAFUGAJI wa kuku nchini wameshauriwa kufuga kisasa na kuacha ufugaji wa mazoea ili kuongeza tija na kujikwamua kiuchumi.

Meneja Masoko wa kitaifa kutoka Silverlands Tanzania limited Taasisi inayojihusisha na ufugaji na uuzaji bora wa vifaranga Bi.Mwanamvua Ngocho amesema hayo leo Agosti 6,2024 kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma. 

Ushiriki wetu hapa nane nane umekuwa mzuri kwasababu tumeona watu wengi wanakuja wanapata elimu ambayo unaona wanahamu ya kupata elimu, 

Kazi yetu kubwa ni uzalishaji wa vifaranga bora na chakula cha kuku vile vile tuna chuo cha mafunzo ya ufugaji kuku bora pale pale Ihemi Iringa.

Amesema Silverlands Tanzania limited inazalisha kuku wa aina tatu ambao ni kuku wa mayai ambae kazi yake ni kutaga tu, kuku wa nyama ambae wengi wanamuita boiler na anakuwa kwa muda mfupi na kuku anaitwa SASO.

Kuku aina ya SASO huyo ndio ambae tunajivunia zaidi yeye yupo kwaajili ya nyama, na tukimshauri mtu afuge kwaajili ya mayai tunamshauri afuge ya nyumbani kwasababu SASO ananenepa sana hafai kwa biashara kwasababu akinenepa utagaji wake unakuwa mgumu 

 amesema

SASO ni kuku ambae anapatikana Silverlands Tanzania limited  pekeake na unaweza ukasema unanunua kuku wa kienyeji kumbe SASO yupo ndani yake,SASO anaanza kutaga akiwa na miezi minne na nusu wakati wa kienyeji anaanza kutaga akiwa na miezi sita

 amesema Mwanamvua

Akizungumzia Kampuni hiyo amesema imeanza kufanya kazi mwaka 2014 na wao wana vizazi mama vya hao kuku wote ambao wanawafuga, vifaranga vyote vinatotolewa Iringa Ihemi na wao wanatoto vifaranga huwa tunatotoresga laki 2 na nusu kwa wiki

Lengo ni kuhakikisha tunatoa huduma bora na niwahakikishie wafugaji watapata vifaranga bora na tutawatengenezea chakula cha wanyama na ni chakula ambacho kitazingatia kiwango cha mataifa lakini pia tunawahakikishia mafanikio yani mtu ukifuga wanakua haraka, hatutii virutubisho ambavyo havikubaliki kama watu wengine wanaoweka booster,ili wakue haraka

 amesema

Silverlands Tanzania Limited iko katika Mikoa 23 nchini na inatoa huduma za uuzaji wa chakula cha kuku na vifaranga bora huku ikiwa imesambaza wafanyakazi ambao wamebobea katika shughuli hiyo.






Post a Comment

0 Comments