SERIKALI KUENDELEA KUTOA ELIMU KWA JAMII KUHUSU MADHARA YA ULEVI

 


📌 RHODA SIMBA

SERIKALI imesema inaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu kupunguza madhara ya ulevi uliopitiliza, unaowafanya vijana  kushindwa kufanya shughuli za uchumi.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 29, 2024 bungeni jijini Dodoma,wakati akijibu swali la mbunge wa Hai Saashisha Mafuwe, aliyeuliza kuhusu kauli ya serikalli juu ya udhibiti wa vileo vinavyoingizwa kiholela na kusababisha kuibuka kwa wimbi kubwa la vijana kulewa wakati wa kazi.

Majaliwa amesema Serikali inao utaratibu unaowezesha kutambua uzalishaji, uuzaji udhibiti biashara inayoingia nchini ya kileo na hivyo inaendelea kusambazwa kwa wateja kwa utaratibu uliowekwa kwa walio na vibali.




Post a Comment

0 Comments