MWITIKIO USAJILI BRELA WAONGEZEKA NDANI NA NJE YA NCHI

 ðŸ“ŒPENDO MANGALA

WAKALA  ya usajili wa biashara na leseni (BRELA) umesema mwitikio wa usajili wa biashara kwa wananchi umeongezeka ndani na nje ya nchi kutokana na watu kuchangamkia masuala ya  uwekezaji.

Hayo yameelezwa Agosti4 katika viwanja vya nanenane Nzuguni Jijini Dodoma na Gabriel Gilangay,Afisa Usajili wa  Wakala huo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambao wameshiriki katika maonyesho hayo.

Gilangay amesema Wakala umekuwa ukitekeleza majukumu mbalimbali ambapo hivi sasa umeanza kuwasajili wakulima ili nao wawe na Nembo  za biashara  ili watambulike.

Kama  Wakala tutahakikisha tunawasaidia wakulima ambao wanalima kibiashara kwa kuwasajili kwa utambulisho wa nembo  maalum ambazo zitawasaidia kufanya kazi zao.,

Wakala tutawapa nembo maalum ya biashara Wakulima ambao watajisajili kwa kuhakikisha tunawapa ulinzi  hasa katika upande wa teknolojia, kwa bidhaa zinazoenda Sokoni inawasaidia wakulima kusajili biashara zao rasmi ili kuwa na usajili wa kampuni, ushirika, au bidhaa ndogondogo zinazohusiana na kilimo. 

Hata hivyo amesema   BRELA imekuwa ikitoa huduma hizo ili kuhakikisha biashara za kilimo zinakubalika kisheria ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za ushauri kuhusu jinsi ya kufuata taratibu za kisheria katika biashara ya kilimo.

Pamoja na hayo, Gilangay ameendelea kutoa wito kwa watu wanaotaka kufanya biashara kuhakikisha wanafanya usajili ili watambulike.

Katika hatua nyingine ametoa wito  kwa wakazi wa Dodoma na nje ya Dodoma kwenda katika Mabanda yao kupata elimu kuhusiana na masuala ya usajili wa biashara.



 

Post a Comment

0 Comments