ITRACOM YAJIPANGA KUSAMBAZA MBOLEA HADI NGAZI YA KIJIJI.

 




📌RHODA SIMBA

KIWANDA cha Mbolea cha Itracom kilichopo Nala jijini Dodoma, kimesema kimeweka Mkakati wa kuwafikia wakulima wote hadi ngazi ya kijiji kwa kusambaza mbolea lengo likiwa ni kuwapunguzia mzigo wakulima wa kufuata mbolea.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya biashara na masoko kutoka Itracom Claudia Kimako, Agosti 3 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kimako amesema, Mkulima hatakuwa na haja ya kusafiri kwenda Wilayani kwaajili ya kununua mbolea na baada ya wakulima wengi kutumia mbolea hiyo, ongezeko la watumiaji litakuwa kubwa kutokana na ubora wake na wao kama kiwanda watahakikisha kwamba kila mkulima anafikiwa.

Sisi kama kiwanda cha mbolea kinachozalisha mbolea hapa nchini na mbolea yetu ni mchanganyiko wa asili na chumvi chumvi ni kwamba wakulima watumie mbolea hizi ili warudishe rutuba kwenye ardhi yao, amesema.

Kiwanda hicho kina aina tatu za mbolea kinachozalisha ikiwemo mbolea ya kupandia,mbolea ya kukuzia pamoja na mbolea ya kukuzia mazao yenye asili ya mizizi.

Akitoa taarifa ya kiwanda hicho Kimako amesema Kiwanda hicho kina viwanda vitatu,viwanda viwili tayari vimeanza uzalishaji na vinauwezo wa kuzalisha tani laki mbili kwa kila kiwanda, ambapo kwa uzalishaji wa viwanda hivyo ni tani laki 4 kwa mwaka pia, kuna kiwanda kimoja ambacho kipo katika majaribio nacho kinauwezo wa kuzalisha tani laki mbili.

Pia kuna viwanda viwili vinavyomaliziwa kufungwa kwahiyo tunategemea hadi mwisho wa mwaka Disemba 2024 tutakuwa na uwezo wa kuzalisha kiasi cha tani milioni moja kwa mwaka,  amesema.

Akizungumzia hali ya usambazaji wa mbolea hizo amesema kuwa mbolea hizo zinasambazwa nchini na nchi jirani.

Tumeshafanikisha kupeleka kenya pia burundi ambapo ndio asilia ya hiki kiwanda na kwa hapa Tanzania tayari tumeshaifikia mikoa 21 na katika maeneo yote mbolea yetu ilipofika matokeo ni mazuri,  amesema.

Kadhalika amesema kuwa, changamoto wanayokumbana nayo nikwamba mbolea hiyo bado mpya hivyo jamii bado hawajaifahamu hivyo wanaendelea kuandaa mashamba darasa kwa wakulima ili waweze kuifahamu mbolea hiyo.

 Hata hivyo Kimako ameelezea kuhusu suala la ajira kuwa mpaka sasa Watanzania 610 wamepata ajira katika kiwanda cha itracom huku warundi wakiwa ni 236.

 


 

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments