📌Na Mwandishi wetu, Morogoro.
MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha
amesema, Mzumbe iko tayari kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi
katika kubadilishana uzoefu katika maeneo ya taaluma na tafiti.
Prof. Mwegoha amesema hayo mwishoni mwa wiki
wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na
Chuo Kikuu cha Bonn yanalolenga kuimarisha uhusiano wa kitaaluma na kuboresha
ubora wa elimu, utafiti na ubunifu baina ya vyuo hivyo.
Awali,Prof. Detlef Mueller-Mahn kutoka Chuo Kikuu cha Bonn amesema ni fursa kwao
kuimarisha ushirikiano utakaoleta tija baina vyuo hivyo kwa kuinua viwango vya
elimu ya juu na utafiti katika nyanja mbalimbali huku ukihimiza uvumbuzi na
ubunifu.
Makubaliano hayo ya ushirikiano yanaelekezaushiriki wa Chuo Kikuu Mzumbe katika miradi ya utafiti na kuboresha mitaala ilikukidhi mahitaji ya soko ya ajira kimataifa. Pia, ushirikiano huo utaleta fursaza semina, warsha na kongamano za kitaaluma zinazolenga kujadili changamoto nambinu bora za kuboresha elimu na utafiti.
Hati ya makubaliano baina ya Chuo Kikuu Mzumbe na
Chuo cha Bonn ni ya miaka mitano kufuatia kukamilika kwa awamu ya kwanza ambapo
wanataaluma wamenufaika na fursa za masomo na tafiti katika nyanja za taaluma
na tafiti.
0 Comments