BALOZI WA SWEDEN NCHINI ATEMBELEA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI KILIMANJARO

 ðŸ“ŒMWANDISHI WETU

JANA Agosti 5 2024 Balozi wa Sweeden nchini Tanzania Mh. Charlotta Ozaki Macias  ametembelea Klabu ya waandishi wa Habari  Kilimanjaro (MECKI) kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na klabu hiyo pamoja na kufanya mazungumzo na wanachama wa mkoa huo.

Mh. Balozi pia ametaka kujua mchango wa MECKI kwa jamii katika kupaza sauti ili kuibua changamoto zilizopo kwenye jamii na namna klabu hiyo ilivyojipanga kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa 2025.

Pamoja na mambo mengine Mhe Balozi na wanachama hao wamejadiliana masuala mbalimbali  ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na namna ya kuandika habari za uchaguzi.

Aidha Mhe. Charlotta ameambatana na timu kutoka Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) iliyokuwa ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji  Kenneth Simbaya




 

Post a Comment

0 Comments