SENYAMULE AELEZEA FURSA ZA DODOMA UJIO WA TRENI YA RELI YA KISASA (SGR)

 


📌RHODA SIMBA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, amesema ujio wa Treni  ya Reli ya Kisasa (SGR) ,utasaidia wananchi kufanya shughuli za uzalishaji mali kwakua muda uliokuwa ukitumika njiani kutoka Dodoma, kwenda Dar es alaam kwa sasa wananchi wanaweza wakafanya shughuli  za kujiingizia kipato.

Senyamule ameyasema hayo leo Julai 30 2024 jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mapokezi ya Trein  hiyo, inayotarajiwa kupokelewa rasmi Agosti 1, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan. 

Senyamule amesema faida zitakazopatikana katika Mkoa wa Dodoma ni pamoja na faida za kiuchumi Kijamii na faida za mtu mmoja mmoja.

Mkoa wa Dodoma kuna faida, mtu anaondoka asubuhi na maboksi yake ya zabibu anaenda Dar es Salaam anauza  biashara  yake na jioni anarudi na faida yake hivyo hivyo hata kwa wafanyabiashara  Senyamule

Tunashuhudia wadau mbalimbali wafanya biashara watajitokeza hapa kama tunavyoona bajaji, bodaboda,nakadhalika ila zipo fursa mbalimbali kwa hapa Stesheni zikiwemo maendeleo ya kufanyia biashara

Senyamule 

 


 

 

 


Post a Comment

0 Comments