TANZANIA INAONGOZA KUHESHIMU UHURU WA VYOMBO VYA HABARI AFRIKA MASHARIKI -WAZIRI NAPE

 

📌MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye (MB), Amesema kuwa Takwimu kutoka Word Press Freedom Index 2024 inayoratibiwa na Taasisi ya  Reporters Without Boarders zimeonyesha kuwa katika nchi za Afrika Mashariki, Tanzania inaongoza  kwa kuheshimu Uhuru wa Vyombo vya Habari ambapo kimtaifa Tanzania imeshika nafasi ya 97 mwaka 2024 ikipanda toka nafasi ya 143 mwaka 2023 na kupelekea kupanda katika kuheshimu Uhuru wa vyombo vya Habari

Mheshimiwa Nape Nanuye ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akisoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolijia ya Habari ya mwaka 2024-2025

Ameongeza kuwa Mafanikio haya yametokana na Serikali kuchukua hatua muhimu ikiwemo Bunge kufanya mabadiliko ya Sheria ya Huduma ya Habari , Sura 229. 

Aidha katika kipimo kingine cha mwezi April 2024 cha Uhuru wa kutoa maoni kwenye Vyombo vya habari cha Afrobarometer, Tanzania imeshika nafasi ya kwanza kwa nchi 39 za Afrika zilizofanyiwa utafiti huo.

Mheshimwa Nape Nnauye pia amevishukuru vyombo vyote vya habari na Jumuiya zake ikiwemo UTPC, MOAT, TAMWA, MCT, MISA Tan, TADIO, TMF, TEF, JOWUTA, JUMIKITA  na JAMII FORUMS kwa kuendelea kuhabarisha Umma wa Watanzania 


Post a Comment

0 Comments