📌MWANDISHI WETU
AFISA
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya WazoHuru Media na Mwanachama wa Klabu ya waandishi
wa Habari Mkoa wa Dodoma Mathias Canal amechangia madawati 20 katika Shule ya Msingi Kiomboi-Bomani iliyopo Wilayani Iramba katika Mkoa wa Singida.
Mathias
amechangia madawati hayo Mei 2024 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali
kuhakikisha vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinaimarishwa na kuhakikisha
kuwa sekta ya elimu nchini inaendelea kuimarika.
Kwa
nyakati tofauti wanafunzi na walimu wa shule hiyo wakiongozwa na Mkuu wa shule
Mwalimu Sadick Mkoma wamemshukuru Mathias kwa kujitoa kwake kwa ajili ya kuunga
mkono juhudi za wazazi pamoja na serikali.
Canal
amesema kuwa serikali inafanya kazi kubwa kwa ajili ya kuijenga nchi hivyo
kupitia sekta mbalimbali ikiwemo elimu wadau wanapaswa kushiriki kuchangia ili
kuimarisha sekta mbalimbali kuunga mkono juhudi za serikali.
Msingi wa maisha na mafanikio madogo niliyonayo ulianzia Shule ya msingi Kiomboi Bomani, wazazi wangu pamoja na wazazi wa hawa watoto wanaosoma Kiomboi Bomani wamenilea na kunivumilia kwa kila namna hivyo njia pekee ya kuwashukuru ni kuwafanya watoto wao wakae kwenye madawati sio chini,
Wakati mwingine tunaweza kuwalaumu wanafunzi kwa utoro au matokeo mabovu darasani lakini kumbe tatizo ni mazingira magumu wanayopitia darasani ikiwemo kukaa chini
Canal
Canal amesema kuwa amepata wazo hilo la kutoa madawati kutokana na kuona jitihada za serikali kuweka miundombinu mizuri ikiwemo ujenzi wa madarasa, imeajiri walimu wa kutosha, hivyo wadau nao wanapaswa kuungana na serikali kwa hali na mali.
0 Comments