JESHI LA POLISI WEKENI MIKAKATI KULINDA USALAMA MTANDAONI-MH SWALE

 ðŸ“ŒEVA GODWIN

MJUMBE wa kamati ya Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Jimbo la Lupembe, Edwin Swale, ameliomba Jeshi la Polisi wapange  mikakati mizuri ya kulinda usalama wa mtandao.

Ameyasema hayo leo 15,Mei 2024,Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambapo amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinauwezo wa kukaa na kudhibiti wizi wa mtandao kwa asilimia zote ikiwa wameweka mikakati mizuri.

Wizi wa mtandao dunia unakwenda mbele sana, zamani wizi ulikuwa unafanyika kwa kutumia nguvu lakini sasa hivi wanatumia mitandao katika kufanya wizi huo, naomba Jeshi la Polisi wapange mikakati ya kulinda usalama wa mtandao

Sasa hivi mabenki mengi wanaibiwa kupitia mitandao, Vyombo vyetu vinauwezo wa kukaa na kudhibiti wizi wa mtandao kwa kiasi kikubwa sana

Hata hivyo ameiomba serikali kupitia Wizara ya Mambo ya ndani katika bajeti hii ya fedha, bodaboda kupunguziwa bei ya leseni.

Mtazamo wangu ni tofauti kidogo, vijana wetu wa boda wengi hawana leseni Maoni yangu wakati wa bajeti ya fedha, ni vyema leseni ya bodaboda ishuke hadi shilingi elfu ishirini

Post a Comment

0 Comments