BANDA LA RFB KUTOKA KWENYE MAONESHO YA SEKTA YA UJENZI YANAYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE JIJINI DODOMA


Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, akifurahia jambo katika Banda la Bodi ya Mfuko wa Barabara, wakati wa Sherehe za Ufunguzi wa Maonesho ya Sekta ya Ujenzi yanayofanyika kwa siku mbili katika viwanja vya bunge jijini Dodoma. Katikati ni Innocent Bashungwa, Waziri wa Ujenzi, akifuatiwa na Mha. Rashid Kalimbaga Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Barabara na Balozi Mha. Aisha Amour Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi.


📌JASMINE SHAMWEPU

Maneja wa TANROADS mkoa wa Songwe, Mha. Selemani Bishanga (Kushoto), akiangalia kwa makini namna mfumo wa ufuatiliaji wa hali ya barabara unaoruhusu kupokea taarifa za hali ya barabara kutoka kwa wananchi unavyofanya kazi, wakati wa maonesho ya Sekta ya Ujenzi yanayofanyika kwa siku mbili katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Katikati ni Emmanuel Mwakajinga Mkuu wa kitengo cha Tehama wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.

 

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, akimsikiliza Mhandisi Rashid Kalimbaga, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Barabara, wakati alipotembelea Banda la Bodi ya Mfuko wa Barabara, katika maonesho ya Sekta ya Ujenzi, yanayofanyika kwa siku mbili katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Kashinde, akizungumza na Mhandisi Jacob Mukasa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi (katikati) na Afisa Mipango Pastory Ushidi wote kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara, wakati alipotembelea Banda la Bodi ya Mfuko wa Barabara kwenye maonesho ya Sekta ya Ujenzi yanayofanyika kwa siku katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Picha na Bodi ya Mfuko wa Barabara








Post a Comment

0 Comments