SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA UPATIKANAJI UMEME - MAJALIWA

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeendelea kuimarisha miundombinu ya upatikanaji wa nishati ya umeme ili kuchochea shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kutekeleza miradi mbalimbali. 

Aidha amesema hadi kufikia Februari 2024, mitambo ya kuzalisha umeme iliyounganishwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa ilikuwa na uwezo wa kuzalisha jumla ya Megawati 2,129.85. 

Majaliwa ameyasema hayo leo April 3, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba kuhusu, mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na Makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya bunge.

Amesema kutokana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na changamoto za upungufu wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme iliyokuwepo kabla ya msimu wa mvua za El-Nino kuanza, hitilafu kwenye mitambo ya kuzalisha umeme pamoja na upungufu wa gesi asilia katika vituo vya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi, umeme uliozalishwa ulikuwa pungufu kwa Megawati 410.

Katika kuimarisha utoaji wa huduma ya umeme nchini katika kipindi cha mwaka 2023/2024, Serikali imekamilisha mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi I Extension wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 185; mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo ambao umewezesha nchi kupata Megawati 27,

Na hivi karibuni Serikali imefanikisha kuanza uzalishaji wa umeme kutoka Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere kutoka katika mtambo wa kwanza kati ya mitambo tisa ambao unazalisha umeme kiasi cha megawati 235. 

Majaliwa 

 

 

Post a Comment

0 Comments