WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema katika
kipindi cha Julai 2023 hadi Januari 2024, mapato ya ndani yakijumuisha mapato
ya Mamlaka za Serikali za Mitaa yalifikia shilingi bilioni 17,188.4, sawa na
asilimia 95.9 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 17,929.8 na ukuaji wa
asilimia 10.0 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2022/2023.
Majaliwa ameyasema hayo leo April 3, 2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba kuhusu, mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na Makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya bunge.
Waziri Majaliwa amesema Kati ya mapato hayo, mapato yaliyokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yalikuwa shilingi bilioni 15,159.8, sawa na asilimia 97.9 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 15,492.7;.
Mapato yaliyokusanywa na Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala na Taasisi za Serikali yalikuwa shilingi bilioni 1,374.5, sawa na asilimia 78.2 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 1,758.3; na mapato yaliyokusanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa yalifikia shilingi bilioni 654.1 ikiwa ni asilimia 96.4 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 678.8
0 Comments