MTENDAJI Mkuu wa Mahakama Profesa Elisante Ole Gabriel
amesema muhimili huo umekuwa wa kwanza kwenye matumizi ya TEHAMA ambapo ofisi
mtandao wamefikia asilimia 99.9 huku akidai ni aibu katika kipindi cha
teknolojia mtu kukaimisha ofisi pindi awapo kwenye majukumu mengineyo.
Profesa Gabriel ameyasema hayo leo April 5, jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu miaka 60 ya Muungano na shughuli ambazo zimetekelezwa na ofisi hiyo.
Kwenye teknolojia Mahakama tuko vizuri zaidi kama nilivyosema Mahakama ya Tanzania kwa sasa ni ya pili baada ya TCRA kwa maana ya Taasisi za umma katika matumizi ya Tehama, hii ofisi mtandao tuko asilimia 99.9 sikumbuki lini nimekaimisha majukumu ya ofisi kwanza ni aibu, kipindi hiki cha teknolojia unakaimisha ofisi mimi nikiwa popote napitisha barua malipo uhamisho na kila kitu
Kama mnavyofahamu hivi karibuni tumeanzisha mfumo wa akili bandia kama mtakumbuka vizuri tuna kile kitu kinaitwa (artificial intelligency/ akili mnemba) tumekuwa taasisi ya kwanza kutumia artificial intelligence maana yake ni kwamba sasa ile hukumu ambayo jaji au hakimu alikua anaandika kurasa 200 sasa anaongea tu akimaliza kuongea anabonyeza kitufe na kinaanza kutafsiri
Gabriel
Amesema wanaoongoza mifumo hiyo ni watanzania na kama nchi imekwenda mbali zaidi kwenye matumizi ya TEHAMA, na kusema kwamba kwenye jengo linalojengwa hapa Dodoma litafungwa roboti.
Roboti litamuelekeza mtu anapotaka kwenda kwani utapotea, jengo ni kubwa mno kwahiyo utakachofanya utasema unataka kwenda wapi kama ni utawala unafuata roboti linakupeleka mpaka sehemu unayotaka kufika
Gabriel
0 Comments