SERIKALI KUHAKIKISHA ZAO LA CHAI HALIFI NCHINI

📌RHODA SIMBA

WAZIRI wa kilimo  Hussein  Bashe amesema  Serikali itahakikisha zao la  chai halifi  hapa nchini na badala yake watafanya mikakati ya kuinua zao hilo ili liweze kufanya vizuri zaidi.

Kadhalika amesema imekataa ombi la kufungwa kwa kiwanda cha Chai cha Mo Enteprises, pamoja na viwanda vingine kwa sababu vitaleta athari kubwa kwa wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda hivyo.

Bashe ameyasema hayo Machi 26/2024  jijini Dodoma katika katika mkutano wa bodi ya chai ambapo amesema kuna athari  za kufunga viwanda kwa watu mbalimbali ambayo wamewekeza hapo, ikiwemo kukosa ajira kwa baadhi ya watu.

Amesema Serikali iko radhi kuchukua mashamba ya chai na kuyaendesha lengo ikiwa ni kuweka sawa sekta hiyo ili iweze kusonga mbele.

Kutokana na hilo Waziri Bashe amesema watakaa nao chini ili kuona kuna changamoto gani zinazowakabili ili waweze kuzitatua na Viwanda visonge mbele.

Hatutakubali kufunga Viwanda, badala yake tutakaa chini na kujadiliana kuona tunafanya nini, kuna changamoto nyingi ambazo serikali wanakutana nazo lakini wanaendelea kuzifanyia kazi ili ziweze kuondokewa

Naye  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Chai Mary Kipeja amesema wakulima wadogo wa zao hilo wanadai sh Bilion 2.8 kwenye Viwanda Jambo ambalo linawarudisha nyuma.

Kipeja amesema fedha hizo ni nyingi ambapo wameiomba Serikali kusimamia hilo ili waweze kupata fedha zao.

Wakulima wadogo wanadai fedha zao kutoka kwa Viwanda, naomba suala hilo lifanyiwe kazi ili wakulima wapate haki yao. Amesema wakulima wanaweka jitihada katika kilimo hicho, lakini wanakatishaa tamaa kutokana na kutokupata fedha zao kwa wakati ili waweze kujikimu wao na familia zao


 

  

Post a Comment

0 Comments