HOJA 22 KATI YA 25 ZA MUUNGANO ZAPATIWA UFUMBUZI

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

SERIKALI kupitia  Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano  na Mazingira imesema jumla ya hoja za muungano 22 kati ya 25 zimepatiwa   ufumbuzi huku tatu zikiendelea kutafutiwa suluhisho.

Hayo yamesemwa leo Machi  26 ,2024 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Selemani Jafo wakati akizungumzia mafanikio yaliyopatikana kuelekea miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Jafo amezitaja hoja ambazo hazijapatiwa ufumbuzi ni mgawo wa hisa unaotokana na sarafu ya Afrika Mashariki, mgawanyo wa faida kutoka benki kuu na uletaji wa sukari wa Kiwanda cha Mahonda katika soko la Tanzania bara. 

Nyingine usafiri wa vyombo vya moto ambayo inataka mtu anapotoka Zanzibar na gari yake aweze kutembea muda wote Tanzania Bara ,Kiujumla ni kwamba tumepata mafanikio makubwa kwa sababu kero zimetatuliwa 22 haya ni mafanikio makubwa sana na hasa katika kipindi cha sasa ufanisi umekuwa ni mkubwa sana

Amesema changamoto nyingi ambazo zilikuwa hazijapatiwa ufumbuzi zimejadiliwa na pande zote mbili za Muungano na kupatiwa ufumbuzi na Kuhusu lini watalimaliza, Dk Jafo amewatoa hofu watanzania kuwa kazi inaendelea vizuri na utashi wa viongozi uko wa hali ya juu.

Amezungumzia mafanikio katika kipindi cha miaka 60 ya Muungano kuwa ni pamoja na huduma za kijamii kama vile elimu, afya, maji, barabara, umeme, utoshelezi wa chakula pamoja na ustawi wa jamii kwa ujumla. 

Hata hivyo Waziri Jafo amesema kwa upande wa huduma za elimu, shule za msingi zimeongezeka kutoka shule 3,270 mwaka 1961 hadi shule 20,562 mwaka 2024 na katika upande wa shule za sekondari nazo zimeongezeka kutoka shule 41 mwaka 1961 hadi shule 6,511 mwaka 2024. 




 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments