SERIKALI YAKIRI KUWEPO UHABA WA SUKARI NCHINI.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

SERIKALI imekiri kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa sukari nchini  huku ikisema upungufu huo umetokana na kuwepo kwa mvua nyingi zilizopelekea kujaa maji katika mashamba ya miwa na kusababisha maeneo ya mashamba ya miwa yanayozalisha sukari wamiliki kushindwa kutoa miwa shambani na kupeleka viwandani. 

Hayo yameelezwa leo Februari 8 bungeni Jijini Dodoma na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbambabay Mhandisi Stellah Manyanya aliyetaka kufahamu kauli ya Serikali kuhusu upungufu wa sukari na ikiwa siku chache kutoka sasa wananchi wanaelekea kwenye kipindi cha mfungo wa kwaresma na Mwezi mtukufu wa Ramadhan. 

Upungufu huu umeshafanyiwa kazi na Wizara Kilimo na tayari Waziri wa Kilimo katoa maelekezo ya Serikali juu ya hatua ambazo imeshazichukua

Upunguvu huu umeshafanyiwa kazi na wizara ya kilimo na waheshimiwa wabunge na watanzania mmepata kumsikia Waziri wa Kilimo akitoa maelezo hapa yanini Serikali tunafanya ili kukabilina na upungufu huu ili watanzania na wananchi kwa ujumla waweze kutumia bidhaa hii,"amesema Waziri Mkuu. 

Amesema Wizara imetoa vibali kwa wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo wazalishaji wa sukari wenyewe kuingiza sukari nchini zaidi ya tani laki moja na zoezi hilo linaendelea na taarifa zilizopo kutoka wizara ya kilimo ni kwamba tayari sukari imeanza kupatikana kutoka nje na hiyo itaendelea kupunguza makali ya kukosekana kwa sukari nchini ili watanzania waendelee kutumia bidhaa hiyo.

Ameongeza kuwa wameendelea kukaa na viwanda kuangalia namna bora ya kupata bidhaa hiyo pale ambapo mvua inapungua ili waendelee kuzalisha ili upungufu huo usiwe wa muda mrefu. 

Kipindi hiki tunaamini kuwa tutafika mpaka kipindi cha ramadhani kwahiyo ndugu zetu waislam watafunga ramadhani na Serikali tunawahakikishia kwamba sukari itakuwepo nchini

Majaliwa.

 

Post a Comment

0 Comments