RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi kwenye
mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola
utakachofanyika Unguja- Zanzibar kuanzia tarehe 4 mpaka 8 Machi, 2024 .
Waziri na Kaiba na sheria Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo bungeni jijini ambapo amesema hiyo ni heshima kubwa kwa nchi kuwa mwenyeji wa Mkutano huo unaotarajiwa kuwaleta nchini kwa pamoja mawaziri wa Sheria wa nchi 56
Balozi Pindi Chana amesema Mkutano huo utahudhuriwa na wageni takriban 300 kutoka nchi 56 wanachama wa Jumuiya ya Madola.
Nawashukuru viongozi wote ambao wameshirikiana bega kwa bega katika kuhakikisha wanasimamia maandalizi ya kazi hiyo kutoka katika pande zote mbili za Muungano yaani Tanzania bara na Tanzania Zanzibar
Nichukue nafasi hii kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuridhia mkutano huu kufanyika nchini kwetu, " Amesema Waziri Chana,
Na kusema kuwa "niwapongeze wataalam wote ambao hata tunavyoongea wapo wakiendelea na maandalizi ya mkutano huu mkubwa ambao pamoja na mambo mengine utatoa fursa ya kuitambulisha nchi yetu na vivutio vyake, "Amesema hata hivyo
Kadhalika Waziri Chana amesema mkutano huo utafungwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Aidha amesema , Mwenyekiti wa Mkutano huu ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland. Amesema Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Ofisi ya RaisKatiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar inaendelea na maandalizi ya Mkutano huo kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola.
Dhima ya Mkutano huu ni “Technology and Innovation: How Digitization Paves the Way for the Development of People-Centered Access to Justice”, amesema huo sio tu utaitangaza nchi ya Tanzania katika anga za kimatifa bali utatumika kama chazo cha mapato ya fedha za kigeni.
0 Comments