NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi amesema katika
kanuni mpya ya mafao iliyoanza kutumika Julai mosi 2022, serikali iliboresha
kiwango cha mafao ya pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu kutoka asilimia 50
hadi 67.
Mhe.Katambi ameyasema hayo
Februari 5, 2024 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa
Segerea (CCM), Mhe.Bonnah Kamoli ambaye amehoji lini kanuni mpya za malipo ya
pensheni kwa wastaafu ya kila mwezi ya kutoka asilimia 50 hadi 67 itaanza
kutumika.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri
Katambi amesema kupitia gazeti la serikali namba 357 la Mei 20, 2022 ilitangaza
kanuni hiyo iliboresha kiwango cha mafao ya pensheni ya kila mwezi kwa
wastaafu.
Amesema kanuni hizo ziliandaliwa
kwa kushirikisha wadau wote (Serikali, Wafanyakazi na Waajiri) kwa lengo la
kufanya maboresho ya pensheni ili kuwianisha mafao ya wanachama na kuifanya
mifuko kuwa endelevu.
0 Comments