📌MWANDISHI WETU-BUNGENI DODOMA
SERIKALI imemuhakikishia mbunge wa Singida Mashariki
Miraji Mtaturu kuwa wataenda kuweka vituo vya kukusanyia maziwa na vifaa vya
kutunzia maziwa katika Mkoa wa Singida ili yasiharibike na hivyo kuvutia
wawekezaji.
Kauli hiyo ya serikali inajibu swali lililoulizwa na
Mbunge Mtaturu ,Bungeni Jijini Dodoma.
Ili serikali iweze kuweka uvutiaji wa wawekezaji katika sekta ya maziwa ni wajibu wake pia kujenga vituo vya kukusanyia maziwa,Je ni nini mpango wa serikali wa kuweka vituo vya kukusanyia maziwa katika Mkoa wa Singida ili kuwavutia wawekezaji katika eneo hilo
Mtaturu.
Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji,Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Excaud Kigahe amesema moja ya maeneo ambayo
serikali ya awamu ya sita inaweka msisitizo sana ni maeneo ya vituo vya
kukusanya maziwa na hasa kuweka vifaa vya kuhifadhia maziwa hayo.
Vifaa hivyo vitasaidia kutunza maziwa,kwa hiyo nimhakikishie mbunge Mtaturu kwamba eneo hili pia tutakuja kuweka vituo hivyo vya kukusanyia maziwa na hasa vifaa hivi vya kutunzia maziwa ili yasiharibike wakati yanasubiri kwenda kwenye viwanda
Naibu Waziri
0 Comments