KUTOKANA
na chamgamoto mbalimbali zinazoyakabiri mashirika yasiyo ya kiserikali likiwemo
suala la ukomo wa kutoa huduma, Msajili wa mashirika hayo Vickness Mayao
amesema kuwa suala hilo ni la kawaida hivyo wanatakiwa kwenda kuhuisha mikataba
yao ili yanaendelee kutoa huduma.
Mayao
ameyasema haya Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha mitandao
mbalimbali inayofanya kazi ya kuleta maendeleo nchini na wizara ya maendeleo ya
jamii jinsia, wanawake na makundi maalumu.
Napenda kutoa rai na kuyahakikishia mashirika haya kuwa hakuna shirika litakalofutiwa kwa sababu ukomo umefika kwa hiyo tutaendelea kutambua michango yao hata kama miaka 10 ya kutoa huduma ikifika
Aidha Mayao ameyataka mashirika hayo kuhakikisha yanaandaa miradi ambayo ni endelevu ili kuweza kujipatia fedha za kuendesha mashirika yao kuacha kutegemea fedha kutoka kwa wahisani.
Kama itawezekana hata kwa udogo wake kuwa na mfuko mdogo wa mashirika haya kwanza lakini tayari serikali imekwisha anza kuyasaidia baadhi ya mashirika madogo hapa nchini
Naye Mkurugenzi wa mtandao wa mashirika binafsi (TANGO) Adamson Msimba amesema lengo la kufanya kikao hicho nikuendelea kuleta maendeleo Kwenye mashirika hayo.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake waliohudhuria
katika kikao hicho kutoka asasi za kiraia Mkoa wa Dodoma Edward Mbogo amesema
wanafanya kazi kwa ukaribu na serikali huku akiongeza kuwa suala la teknolojia
limekuwa likileta mkanganyiko katika ulipaji wa kodi kwa mashirika hayo
0 Comments