WAJUMBE TUME YA ULINZI TAARIFA BINAFSI WAASWA KUTUNZA SIRI ZA WANANCHI

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

SERIKALI imezindua Bodi ya Tume ya Ulinzi wa taarifa binafsi huku ikiwataka wajumbe wa bodi hiyo kutunza siri za wananchi.

Kadhalika imewataka wajumbe hao kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo yao badala ya kufuata matakwa ya watu wengine.

Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari Nape Nnauye ameyasema hayo leo Januari 19 wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mpya ambapo amesema tume hiyo mpya inajukumu la kulinda heshima, haki na utu kwa kuhakikisha taarifa za watanzania na hata wageni taarifa zao kuwa sehemu salama na zinatumika kwa kujali haki heshima na utu ili watu waone Tanzania ni taifa salama kwa huduma za kidigitali.

Amesema, wajumbe hao wameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na alivyowaamini huku akiwataka kutekeleza majukumu yao kulingana na walivyoaminiwa.

Wito wangu kwenu ni kuilinda imani ya Rais wetu kwani mchakato wa kuwapata ninyi ulikuwa mkubwa kwa sababu tulijua tunawakabidhi jukumu kubwa la kulinda taarifa zetu.

Waziri Nape pia amewataka wajumbe wa Bodi hiyo kuitangaza Tume hiyo ili iweze kufahamika na wananchi .

Katika nchi yetu hili ni jambo lisilozoeleka ni rahisi watu kutolitumia, kwa hiyo mnapaswa kulitangaza na kutoa elimu kwa umma kuhusu uwepo na majukumu ya Tume kwani kwa sasa bado hawafahamu uwepo wa tume hii

Hivyo mjipange kusimamia suala hili ikiwa ni pamoja na kuandaa makongamano ya kikanda na kimataifa tuwakaribishe na wenzetu watupe uzoefu wao hii itawezesha upatikanaji wa fursa mbalimbali pamoja na kuvutia wawekezaji."amesema na kuongeza kuwa

Tunafahamu watu wengi wamekuwa wakati fulani wakisitasita kuja kuwekeza kwa kukosekana kwa sheria na taasisi huru, na sasa ni jukumu letu kuwajulisha kwa vitendo kuwa Tanzania iko tayari kwamba tumeweka sheria ambayo inakubalika, tumeweka tume iko huru na imekubalika na tupo tayari kuwaonyesha kwamba Tanzania ni salama.

Ameitaka Bodi hiyo kuandaa mpango mkakati na namna bora ya kutoa huduma kwa viwango vya kimataifa huku akisema hatarajii kupokea malalamiko kuhusu utoaji wa huduma, tunataka viwango viwe vya kimataifa .

Pia ameitaka bodi hiyo kusimamia na kuhakikisha watumishi wa tume wanajengewa uwezo mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia na kudumisha ushirikiano.

Hapa Katibu Mkuu na wote mnaohusika na 'recruitment' ya Tume mtafute 'the top cream 'ndio waje kufanya kazi ya Tume, msiweke watu ambao tuna mashaka nao maana hapa kila mtanzania anaguswa na hii Tume, kwahiyo msikimbilie kujaza nafasi tulieni mpate watu wazuri.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ulinzi wa Tume ya Taarifa Binafsi Balozi Mohamed Adadi Rajabu ameahidi kwamba Bodi hiyo itafanya kazi na kutimiza matarajio ya kuteuliwa kwao na kwa mujibu wa maelekezo ya Waziri .

Kikubwa ni kuelewa sheria namba 11 inaeleza majukumu ya tume inataka nini, majukumu ya tume inawataka kutunza Siri za watu taarifa za watu binafsi zinatunzwa


 

 

Post a Comment

0 Comments