TANZANIA YAPATA MSAADA WA TRILIONI 1.4 KUTOKA GLOBAL FUNDS.

📌JASMINE SHAMWEPU

TANZANIA imesaini  mkataba na Global Funds (Mfuko wa Dunia) ambao utatoa msaada wa dola milioni 606.9 za kimarekani sawa na Sh Trilioni 1.4 kwa ajili ya kupambana na maradhi matatu ya UKIMWI,  Kifua Kikuu (TB) na malaria kwa kipindi cha miaka mitatu nchini.

Akizungumza baada ya kusaini mikataba minne, Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba Jijini Dodoma  aliwataka watendaji katika wizara mbalimbali wazitumie kwa wakati na malengo yaliyokubaliwa.

Fedha hizi ni nyingi sana zikatumike kwa uadilifu, kwa kuzingatia maadili na kwa uzalendo kwa malengo yaliyokusudiwa

Wizara zitakazotumia fedha ni pamoja na afya, Tamisemi, ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na maendeleo ya jamii ambazo zinaingia kwenye programu ya utekelezaji miradi hiyo.

Akizungumza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu pamoja na kuwashukuru Global Funds kwa kuipa msaada wa fedha sekta ya afya ambazo zitaisaidia kuokoa maisha ya Watanzania nchini.

Kwa upande wa mapambano na maradhi ya UKIMWI wakati imebaki miaka sita kukamilisha lengo la sita la Maendeleo endelevu, asilimia 75 ya fedha kununua vifaa vya kinga.

Pia fedha hizo zitatumika kusaidia watanzania milioni 1.6 wenye maambukizi kupata ARV vidonge vya kufubaza makali ya Ukimwi katika kila mwaka.

Pia zitatumika kuhimiza wanaume kupima kujua hali zao bila kutegemea majibu ya wenzao wao.

Kuhusu malaria, kuwafikia watanzania milioni 10 kupata matibabu ya malaria kwa miaka mitatu na kutumia kipimo cha haraka cha malaria na kupata dawa mseto mbalimbali bure.

Lakini pia fedha hizo zitasadisa pia katika kugawa vyandarua milioni 22.6 kwa waja wazito, watoto wa chini ya miaka mitano na watoto katika shule.

Kuhusu kifua kikuu (TB) fedha hizo zitatumika katika kuibua wagonjwa wapya wa ugonjwa huo nchini.

Pamoja na kusaidia mapambano dhidi ya malaria, TB na Ukimwi pia zitatumika katika kuimarisha mifumo ya afya katika maeneo mbalimbali nchini.

Mwakilishi wa Global Fund, Linden Morrison alisema Tanzania ni nchi ya nne kwa kupokea fedha kutoka mfuko huo kutokana na kutumia vizuri fedha zinazotoka kwenye mfuko huo.

Taasisi imetoa fedha hizo kwa lengo la kusaidia kufikia malengo ya kitokomeza UKIMWI 2030.




 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments