MUDA WA VIKAO VYA BUNGE WAONGEZWA KUFUATIA MISWAADA ILIYOPANGWA KUJADILIWA.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeanza vikao vyake leo Januari 30 2024, huku likiongeza muda wa wiki 3 kufuatia uzito wa majukumu yaliyopo ikiwemo miswaada ambayo imepangwa kujadiliwa.

Aidha miswaada hiyo iliyopangwa kujadiliwa katika mkutano huo ni Muswaada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais Wabunge na Madiwani wa mwaka 2023 na Miswaada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa mwaka 2023.

Miswaada mingine itakayojadiliwa ni Muswaada wa Sheria ya Marekebisho ya sheria za vyama vya Siasa wa mwaka 2023 na Muswaada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali no.5 wa mwaka 2023.

Kadhalika katika mkutano huo maswali ya wastani wa 250 ya kawaida na maswali 24 ya papo kwa papo kwa Mhe. Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa na wabunge.

 

Post a Comment

0 Comments