WAZIRI wa Ujenzi Innocent Bashungwa
ameziagiza Taasisi zilizopo ndani ya Wizara hiyo kuwajengea uwezo wakandarasi
wa ndani ili kuipunguzia mzigo Serikali kutumia fedha nyingi kwa kuwatumia
wakandarasi wa nje kwaajili ya ukamilishaji wa majengo.
Amesema kutumia wakandarasi wa nje katika umaliziaji wa majengo na kuacha wa ndani, kunaisababishia Serikali kutumia fedha nyingi kuleta watalaam hao.
Bashungwa ameyasema hayo leo Januari 29 jijini Dodoma wakati wa ziara ya kukagua jengo la Wizara hiyo ilioenda sambamba na zoezi la upandaji miti
Katika hatua nyingine Bashungwa ameiagiza Wakala wa barabara nchini Tanzania (TANROADS) kuhakikisha wanaitunza miti iliyopandwa pembezoni mwa barabara ya Iyumbu Chimwaga kama ilivyoagizwa na Makamu wa Rais Dkt Isidori Mpango.
Nae Msanifu wa majengo kutoka Wakala wa majengo Tanzania ( TBA ) Weja Ngo'lo amesema ujenzi huo kwa sasa upo katika hatua za umaliziaji.
Amesema jengo hilo kwa asilimia 68 linajengwa na wazawa ambao wapo chini ya Wizara ya Ujenzi lakini pia TBA wapo kama washauri waelekezi wa mradi huo.
Ni moja kati ya majengo makubwa ndani ya mji wa Serikali tunashirikiana na Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Wizara ya Ujenzi na tuna watumishi wengi
Nae Mkuu wa Vikosi vya Ujenzi Eng.Simeo Machibya amesema mshauri mwelekezi wa jengo hilo ni TBA, na TEMESA na tayari mpaka sasa wamepima ubora wa nyaya TBS kwaajili ya kuvuta jengo zima na wamelipwa asilimia 52 sawa na bilioni 15.
Vifaa vyote vya umaliziaji vimeshaletwa na asilimia kubwa vinatoka nje ukizingatia vioo na mfumo wa Dodoma ulivyo majengo hayo ni marefu na kuna upepo na vifaa vyote vimetoka kwenye viwanda vya ndani hapa na tunaweza kupata na fundi kutoka sehemu yoyote nchi nzima
|
0 Comments