WANANCHI WAIOMBA SERIKALI KUJENGA UZIO SHULENI

 ðŸ“ŒJOYCE  KASIKI

KUFUATIA shule ya msingi Mlezi kupitiwa na barabara kubwa pamoja na kuzungukwa na makazi ya watu, jamii imeiomba Serikali kujenga uzio katika shule hiyo ili kuwanusuru wanafunzi  hasa wale wa darasa la awali hadi darasa la tatu na wale wenye mahitaji maalum kutoroka na kupotea.

Moja ya mambo ya kuzingatia katika suala zima la malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto hasa watoto wenye umri wa miaka sifuri hadi minane, ni ulinzi na usalama wao katika maeneo yote yanayowazunguka ikiwemo shuleni.

Pamoja na ulinzi na usalama wa mtoto, mambo mengine ya kuzingatia ni pamoja na kuhakikisha mtoto anakuwa na afya bora, lishe ya kutosha, malezi yenye mwitikio na ujifunzaji wa awali .

Wakizungumza na mwandishi wetu, wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka shule hiyo wamesema, kujengwa uzio katika shule hiyo itasaidia katika suala zima la ulinzi na usalama wa watoto hasa wale wadogo.

Shule hii ya Mlezi ni moja ya shule zilizopo katika jiji la Dodoma ambayo inafundisha pamoja na watoto wenye mahitaji maalum (Kitengo), lakini pia mazingira ya shule ipo barabarani na imezungukwa na makazi ya watu kitu ambacho ni hatari sana kwa watoto wadogo wa darasa la awali na wale wenye mahitaji maalum, ombi langu kwa serikali ni kujenga uzio katika shule hii ili kuwa na ulinzi wa watoto hao.

Mwanaidi Juma

Naye Anthonia Joseph amesema, kutokana na mazingira ya shule hiyo yalivyo, watoto wamekuwa wakitoka nje ya shule na kufuata mahitaji yao katika maduka yaliyo nje ya shule kitu ambacho hakileti afya katika usalama wao.

Naye Mstahi Meya wa Jiji la Dodoma Prof Davis Mwamfupe amesema, Halmashauri ya Jiji hilo inatambua na inajali usalama wa watoto  hasa ambao shule zao zipo katika maeneo hatarishi ikiwemo barabarani, karibu na masoko, zilizo karibu na hospitali pamoja na zilizo karibu na maeneo ya maegesho ya magari.

Tunajali usalama wa watoto na suala la uzio tunaona lina umuhimu mkubwa wa usalama wa watoto wetu, kwa hiyo wa kuzingatia hilo tutakeleza ujenzi kwa shule moja baada ya nyingine.

Prof.Mwamfupe

Post a Comment

0 Comments