MKUU wa Wilaya
ya Dodoma Mjini Jabiri Shekimweri amewataka wafanyabiashara nchini kumuunga
mkono Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye matarajio makubwa na maendeleo ya
nchi kwa kulipa kodi na kwamba maendeleo hayawezi kufikiwa bila watu,
wafanyabiashara kulipa kodi.
Kadhalika amewata kuwa wabobezi kwenya ajenda ya ulipaji kodi kwa kutumia Mashine za risiti za Kielektroniki (EFD), lengo likiwa ni kutunza kumbukumbu za mauzo huku akiwaomba wafanyabiashara hao kuwahamasisha wengine ambao hawazitumii mashine hizo.
Shekimweri ameyasema hayo leo Disemba 5 jijini Dodoma katika siku ya kipekee na ya shukurani kwa walipakodi wa Dodoma kwa kuwatambua mchango wafanyabiashara walioutoa kwa Serikali na Mkoa katika mwaka wa fedha 2022/2023, iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),amesema kutokulipa kodi ni kujidhulumu.
Amesema kuwa hivi karibuni walikuwa na baraza la biashara mkoani hapa moja ya hoja zilozungumzwa ni kuanguka kwa biashara ambazo zinafanywa kienyeji kwa kukwepa kulipa kodi.
Amesema kuwa moja ya hasara za kutokulipa kodi ni kushindwa kupata mikopo mikubwa kutoka katika taasisi za kifedha.
Kama mtu unakwepa kulipa kodi huwezi kuzipata fursa za kukopeshwa kwa kuwa unakwepa kodi, kiuhalisia unatakiwa ukopeshwe milioni 100 lakini huwezi kupata ndio maana unakuta mtu anabaishara hiyo hiyo miaka 10 hawezi kubadilika
Kutokulipa kodi ni kujidhulumu wewe mwenyewe hivyo tuhamasishane sote na kujenga tabia zaidi ya kulipa kodi kuliko kupingana na sheria," amesema Mkuu huyo wa Dodoma Shekimweri.
Naye Meneja wa Mamlaka hiyo Mkoa wa Dodoma Castro John amewataka wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati ambapo mwezi Disemba ni wa kulipa kodi awamu ya nne na kwamba ifikapo 31, mwezi huu wafanyabiashara hao wawe wameshalipa kodi.
Amesema kuwa wafanyabiashara ni sehemu ya mchakato wa maendeleo ya Taifa na kwamba wasipokuwa timu moja katika ulipaji kodi nchi haiwezi kusogea mbele kiuchumi.
John amesema Mkoa wa Dodoma unajivunia kuwahudumia walipakodi na wafanyabiashara huku akisema ofisi zao zipo wazi muda wote na kwamba endapo wanachangamoto wafike ili kuzungumza.
Kwa wale wenye changamoto ya matumizi ya mashine za EFDs waje tuzungumze, matumizi ya mashine hizi ni muhimu kwa kutunza kumbukumbu na kuleta makadirio ya kodi sahihi
Ameongeza kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya wafanyabiashara kulalamika kodi kubwa na wanapoambiwa wapeleke kumbukumbu zao wanakuwa hawana na kwamba matumizi ysahihi ya mashine hizi yanasababisha makadirio kuwa sahihi.
Leo ni siku ya kipekee ni ya shukurani kwa walipakodi wa Dodoma kwa kuwatambua mchango wa wafanyabiashara hawa walioutoa kwa serikali na Mkoa katika mwaka wa fedha 2022/2023 lakini pia niwashukuru waandishi wa habari tumekuwa tukifanya kazi pamoja
Ameongeza kuwa siku hiyo ni muhimu kwa TRA ambayo inawatambua walipakodi ambapo asubuhi walifanya matembezi ya shukurani kwa ajili ya wafanyabiashara hao na kufuatiwa na hafla fupi jioni ya kuwatunuku waliofanya vizuri katika suala la ulipaji kodi.
Meneja huyo amesema kuwa wafanyabiashara wote mkoani hapo wamefanya vizuri katika ulipaji kodi na kwamba watakaotunukiwa ni wale waliofanya vizuri zaidi ili iwe chachu kwa wengine.
Kwa upande wake mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoa wa Dodoma Joseph Chowa alimpongeza Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kufanya mazingira rafiki kwa wafanyabiashara ya ulipaji wa kodi.Tunaomba matumizi sahihi na mazuri ya vitendea kazi vya ukusanyaji kodi kama mashine za EFDs kusaidia kuleta taarifa zetu ili kuepuka malalamiko ya kodi zinazotukabili
Aidha mfanyabiashara huyo aliwashauri wafanyabiashara wengine kutimiza majukumu yao ya kulipa kodi sahihi inayostahili na kuacha kukwepa ulipaji wa kodi hiyo huku akifafanua kuwa kodi ni jukumu la mfanyabiashara yoyote katika kujenga Taifa kwa pamoja.
Kaimu Mkurugenzi Mirembe Innocent Mungoki amesema wamefarijika kuona TRA inawafikia walengwa na wanaishukuru serikali kwa mwaka wa fedha suala la Afya limepewa kipaumbele na TRA nao wanaendelea kuonyesha kwa vitendo.
Kwa kuzingatia maadhimisho ya siku ya mlipa kodi tumeona siyo vibaya kuhakikisha tunawafikia ndugu zetu ili na wao waone ni sehemu ya jamii na tumewaletea zawadi mbalimbali
Meneja Mkoa TRA Dodoma Castro John.
0 Comments