NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamisi Hamza Khamisi ametaka fedha zitengwe ili kuhakikisha changamoto ya uhifadhi wa Mazingira na mapambano dhidi ya mabadiliko na athari ya tabia nchi kwani ni janga la dunia
Haya ameyasema jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Ukusanyaji wa Mapato ya ndani kwenye sekta ya uzinduaji unavyoweza kufadhili mabadiliko ya tabia nchi ambapo Naibu Waziri huyo amesisitiza na kutaka fedha zinazokusanywa kwenye ripoti hiyo zijielekeze kwenye kampeni za kitaifa za Mazingira kama vile kampeni ya soma na mti.
Amesema fedha zitakapopatikana kwenye sekta ya Gesi, Nishati na Madini zielekezwe na ziendeleze kampeni za serikali zilizoanzishwa za kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiko ya tabia nchi.
Nchini kwetu tatizo la uharibifu wa Mazingira lipo kwa kiasi kikubwa na hiyo yote ni kutokana na uelewa mdogo kwa wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa Mazingira na ndio maana wanajikatia miti hovyo hawalihurimii taifa wao wanaamini ni jambo la kawaida ni wajibu hawakosei
Ripoti hii iende ikatoe elimu katika jamii umuhimu wa kupanda na kutunza miti na Mazingira kwa ujumla, tusipofanya hivyo vizazi vijavyo vitakuja kujua kuwa asilimia kubwa ya Tanzania ni jangwa kumbe ni kutokana na ukataji wa miti
Naibu Waziri Khamisi
Pia ameekeza ripoti hiyo ijikite kwenye Utunzaji wa vyanzo vya maji kwani bado kuna changamoto watu wanachepusha maji wanatoa maji katika asili yake na kupeleka mashambani kwao.
Amesema watu wamesahau sheria ya Mita 60 wanalima karibu na mito wanatumia mbolea za sumu zinakwenda kwenye vyanzo vya maji na kupelekea viumbe hai wengine kufa au kupotea kwenye Mito.
Sasa Ripoti hii ihimize na kuzungumza juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji kwani ukweli ni kwamba Mito ni maisha yetu
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Policy Forum Christina Ruhinda amesema wanachama wa Policy Forum wapo kwenye taasisi mbilimbali ambazo zinashughulikia masuala yanayohusu sekta zote hapa nchini.
Amesema wanachama wanagusa mipango yote na kushiriki katika utekelezaji ili kuhakisha Tanzania inafikia maendeleo yaliojipangia kimkakati kuyafikia na kuchangia katika ukuaji na kuhakisha uwajibikaji na ufanyaji kazi kwa watu wote.
Naye Makupa Nsenduluka Afisa Sera Kodi na Usimamizi wa Rasilimali amesema kama ilivyo kwa nchi nyingi zinazoendelea, Tanzania imeathiriwa sana na mabadiliko ya tabianchi madhara ambayo hayaishii tu kusababisha mafuriko na ukame lakini yanaharibu Miundombinu na hata kuathiri maisha ya watanzania.
0 Comments