WIZARA
ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Wizara ya ardhi Nyumbani na Maendeleo
ya Makazi imetakiwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi pamoja na miongozo ya
Benki ya Dunia (WB) wakati wa kutekeleza mradi wa uboreshaji usalama wa miliki
ardhi (LTIP).
Maagizo
hayo yametolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry
Slaa, wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri mkuu, Kassim Majaliwa kwenye
mkutano wa kitaifa wa wadau kujadili utekelezaji mradi wa uboreshaji usalama
miliki za ardhi.
Amesema
Januari 21, 2022 serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi ilisaini makubaliano na Benki ya Dunia ya mkopo wa Sh.bilioni 346 sawa
na dola za kimarekani milioni 150 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Mradi huu unatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano na una vipengele vinne ambavyo ni kuongeza usalama wa milki,kuimarisha mifumo ya taarifa za ardhi, kujenga miundombinu ya ardhi na usimamizi wa mradi
Aidha,
amesema mradi huo utatoa fursa mbalimbali katika makundi yote ya kijamii kwa
kuzingatia makundi maalum na kuleta usawa wa kijinsia.
Na kuwezesha wamiliki wa ardhi kumiliki ardhi zao kisheria na hivyo kupunguza migogoro mbalimbali inayohusiana na matumizi ya ardhi hasa ya wakulima na wafugaji pamoja na maeneo yaliyotengwa kwa shughuli maalumu
Amesema
vipengele vya mradi vikisimamiwa vyema vitaleta mchango mkubwa katika maendeleo
ya kijamii, kiuchumi na mazingira katika maeneo mengi.
Pia,
amesema mradi utaimarisha haki za umiliki ambao utachangia kukuza uwekezaji na
maendeleo ya kiuchumi, kuongeza uzalishaji na usalama wa chakula, kupunguza
migogoro ya ardhi na kukuza utunzaji wa mazingira.
Moja ya vitu vikubwa vitakavyofanywa na mradi ni ujenzi wa majengo 25 ya Ofisi za ardhi za mikoa, ofisi hizi zote zitawezeshwa kufungwa mfumo wa kielektroniki wa usimamizi na utekelezaji wa kazi za ardhi
Hata
hivyo, amesema mifumo hiyo itaongeza ufanisi, uwazi na uhakika katika taratibu
za umiliki wa ardhi kwa kusaidia kuhifadhi kumbukumbu, kulinda taarifa na kuboresha
mchakato wa umiliki wa ardhi.
Amesema
ili mradi huo ufanikiwe ni muhimu wadau kushiriki kikamilifu katika utekelezaji
wake,
Niendelee kuwaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zinazotekeleza mradi kutoa ushirikano kwa timu za utekelezaji wa Mradi.
Aidha, taasisi zinazofanya kazi karibu na mradi zikiwemo NIDA, NEMC,Tume ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Vyuo vya Ardhi na Taasisi nyingine zote kutoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa mradi
Pia,
amewaagiza wakurugenzi wa halmashaurii nchini katika kipindi cha maandalizi ya
bajeti ya mwaka 2024/25 watenge fedha kwa ajili ya sekta ya ardhi ili
kuendeleza utekelezaji wa mradi katika maeneo yale ambayo mradi haujaweza
kufika.
Vile
vile, amewataka watalaam wa sekta ya ardhi washirikiane na viongozi wa serikali
za mitaa na vijiji kuwapa wananchi elimu kuhusu masuala ya ardhi hususan
taarifa za utekelezaji wa mradi huo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Antony Sanga, amesema
tangu utekelezaji wa mradi uanze, Machi, 2023 hadi sasa mradi ukishirikiana na
wilaya na halmashauri husika umepata mafanikio mbalimbali mijini na vijijini.
Amesema,
mafanikio hayo ni pamoja na kazi za upimaji na umilikishaji wa ardhi kwa upande
wa vijijini unaendelea katika halmashauri za wilaya tano ambazo ni Tanganyika,
Mufindi, Maswa, Mbinga, na Songwe.
Jumla Tsh. 270,255,481/= zimekusanywa kama maduhuli ya Serikali yatokanayo na ardhi katika kipindi cha kuanzia Septemba 2023 hadi sasa
Sanga
Hadi kufikia Tarehe 20 mwezi huu wamiliki wa vipande vya ardhi 122,045 wametambuliwa vijijini na tayari Hatimilki za kimila 10,568 zimeandaliwa na kusajiliwa katika mfumo wa usimamizi wa ardhi
0 Comments