Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Mhe. Mwanaisha Kwariko akifungua mafunzo kwa watendaji hao yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya. |
📌MWANDISHI WETU
TUME ya Taifa ya Uchaguzi imewataka Watendaji wa Uboreshaji wa Majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara kuweka utaratibu mzuri utakaoviwezesha vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi kushiriki katika uboreshaji katika Kata ya Ikoma.
Akifungua
mafunzo kwa watendaji hao yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya
Wilaya ya Rorya, Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Mhe.
Mwanaisha Kwariko alisema vyama vya siasa vinaruhusiwa kuweka mawakala katika
uboreshaji huo.
Amewataka
watendaji hao kuvishirikisha vyama vya siasa katika masuala yote ambayo
wanastahili kushirikishwa kwani jambo hilo litawarahisishia utekelezaji wa
majukumu yao katika uboreshaji huo.
Niwakumbushe kuwa, vyama vya siasa vinaruhusiwa kuweka mawakala katika vituo vya uandikishaji. Nitumie nafasi hii kuwasisitiza kuweka utaratibu mzuri utakaoviwezesha vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi kushiriki kikamilifu katika zoezi hili
Jaji wa Rufaa Mhe. Mwanaisha Kwariro.
Mjumbe huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi alitoa wito kwa watendaji hao wa uboreshaji wa majaribio kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maelekezo ya Tume watakayopewa.
Vilevile mhakikishe mnasimamia utunzaji wa vifaa vyote vitakavyotumika katika zoezi hili kwani vimenunuliwa kwa gharama kubwa
Jaji wa Rufaa Mhe. Mwanaisha Kwariko.
Mafunzo hayo kwa
watendaji wa uboreshaji wa majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unajumuisha
Mratibu wa Uandikishaji wa Uchaguzi wa Mkoa wa Mara, Afisa Mwandikishaji wa
Jimbo la Rorya, maafisa waandikishaji wasaidizi, maafisa ugavi, maafisa TEHAMA
na maafisa wanaoshughulikia masuala ya uchaguzi katika Jimbo la Rorya.
Tume ya Taifa ya
Uchaguzi itafanya uboreshaji wa majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
katika Kata ya Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Mkoa wa
Mara na Kata ya Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa
wa Tabora, kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa watendaji hao yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, wakisaini viapo kabla ya kuanza mafunzo. |
0 Comments