WANANCHI WAPEWE TAARIFA ZA SERIKALI

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

WATENDAJI wa Serikali wametakiwa kutokuwa wachoyo wa kutoa taarifa zinazowasaidia wananchi kwakua ni jukumu la kila Mtanzania kujua kinachofanywa na serikali yao.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari Mhe.Nape Nnauye ambapo amesema utoaji wa taarifa za maendeleo ni kuonyesha kwa uhalisia uwajibikaji wa serikali yao ambayo wanailipia kodi wakati wakipatiwa huduma mbalimbali za kijamii, hivyo lazima kujua kodi zao zinatumikaje katika kuinua taifa.

Amesema “wananchi wanataka kujua kodi zao zimewasaidiaje katika huduma mbalimbali zikiwemo sekta ya maji, nishati, kilimo, miundombinu na shughuli zingine za maendeleo kwa jamii” amesema Mhe.Nape

Amesema kuna mambo mengi ya maendeleo nchini wananchi hawayajui kutokana na sababu mbalimbali hivyo ni vyema kuhakikisha wananchi wanapatiwa taarifa mbalimbali, hivyo viongozi na wananchi washirikiane katika kujua kinachofanywa na serikali.

Nae  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule  amesema kuwa Serikali imetoa zaidi ya Shilingi bilioni 81 Kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya sekta ya Elimu katika mkoa wa Dodoma ambapo imejenga Madarasa mapya zaidi ya 1400 na Shule mpya kabisa 124 na kupelekea ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza na tano kuongezeka.

Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Dkt.Samia imeufanyia mambo makubwa mkoa wa Dodoma kuanzia sekta ya afya, Elimu, barabara na maeneo mengine hivyo ndani ya miaka hii mitatu mkoa wa Dodoma unaendelea kwa kasi katika sekta zote tunamshukuru sana

Senyamule 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Dkt.Festo Dugange ametoa maelekezo kwa Wakuu wote wa Mikoa 26 Nchini kuhakikisha wanatoa taarifa ili wananchi wafahamu kazi inayofanywa na Serikali.

Kadhalika Dugange ametoa maelekezo kwa wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote nchini kutoa ushirikiano katika utoaji wa taarifa wa miradi mbalimbali inayofanywa ziwafikie waandishi wa habari ili ziweze kufika kwa jamii.

Suala la utoaji wa taarifa hizi uwe wa lazima na wa mara kwa mara ili wananchi wajue kazi inayofanywa na serikali yetu inaonekana kuna gape katika eneo hili Nisisitize  na tutaendelea kufuatilia kuhakikisha jambo hilo linatekelezwa

Dugange amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itafanya utaratibu wa kuhakikisha kila Halmashauri inapata afisa habari ambaye amekamilika na vitendea kazi kwaajili ya kutoa taarifa za Serikali na viongozi wahakikishe wanakuwa nae katika kila kikao kufahamu yanayoendelea.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali amewataka watendaji wa serikali kutowanyima taarifa wananchi za maendeleo kwakua wanachangia fedha kupitia kodi mbalimbali hivyo ni vyema wananchi wakajua kile kinachofanywa na serikali yao.





 

Post a Comment

0 Comments