📌RHODA SIMBA
WANANCHI wameshauriwa kuendelea kushiriki kwenye tafiti za takwimu zinazofanywa na Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), kwa kutoa majibu sahihi pindi wanapoulizwa kwa kuwa majibu hayo ndiyo yanayoipatia nchi takwimu sahihi na bora.
Akizungumza Jijini Dodoma na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika ambayo hufanyika Novemba 18, kila mwaka, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya watu na takwimu za jamii Ruth Minja amesema kuwa takwimu bora ndio huzaa mipango na programu zinazojibu changamoto za maendeleo.
Minja amesema kuwa wananchi wakifanya hivyo watakuwa wamesaidia kuharakisha maendeleo yao binafisi na nchi kwa ujumla.
Ameongeza kuwa hapa nchini maadhimisho hayo yalianza tangu Novemba 13, mwaka huu kwa shughuli mbalimbali za kitakwimu na kwamba yatahitimishwa Novemba 21 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.
Kaimu huyo amesema lengo la maadhimisho hayo ya Takwimu Afrika ni kuelimisha wadau wote pamoja na wananchi wa bara la Afrika kuhusu umuhimu wa takwimu rasmi na kuhumiza matumizi yake katika nyanja za maisha kiuchumi, kijamii na kimazingira.
Ni kawaida maadhimisho haya ya Takwimu Afrika kuwa na ujumbe maalamu ama kaulimbiu ambayo ndio inatoka dira ya maadhimisho na mwaka huu 2023 kaulimbiu ya tunaadhimisha siku ya Afrika inasema "Uboreshaji wa Mifumo ya Ushirikiano wa Kitakwimu ili Kuharakisha Utekelezaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika ( African Continental Free Trade -Area- AfCFTA) Mchango wa Takwimu Rasmi na 'Big Data' katika mageuzi ya Kiucumi na Maendeleo na Endelevu ya Afrika
0 Comments