MWENYEKITI wa Chama Cha Wafugaji Tanzania
(CCWT) Mrida Mshote amewataka wafugaji kupeleka watoto shule, kufuga kisasa na
kuachana na desturi ya kuwa na mifugo mingi lakini mazingira ya maisha yao kuwa
ni duni.
Mrida ameyasema hayo leo Novemba 17 Kilosa, Mkoani Morogoro kwenye mkutano na wanachama wa CCWT wenye lengo la kuwasajili wafugaji kwa kadi za kielektroniki, teknolojia ambayo inaaminika itasaidia katika kufahamu taarifa husika za wafugaji na idadi yao.
Kwa mfano mimi ni mfugaji ambae kila mwaka nauza mifugo ili kupata huduma zingine za kijamii na napunguza ili nibaki na mifugo ambayo nina imudu katika malisho na huduma ya kuweza kuwasomesha watoto wangu
Mrida
Kadhalika amewataka Wafugaji kuwa na ushirikiano na wakulima na kusema kwamba maisha yao wanategemeana.
Unakuta mtu mpaka anaua kisa ng'ombe ameambiwa ameingiza kwenye shamba la mtu na hataki kukubali kosa, Ndugu zangu tusifike huko kwenye kuuana damu ya mtu itakutesa hata kama si ndugu yako tufuge mifugo ambayo tunaweza kuihudumia kwenye malisho
Pia niwaombe wafugaji mjisajili ili wanapozungumzia wafugaji kuwe na wafugaji waliojiandikisha lengo Serikali iweze kutuhudumia kwa kuwa na takwimu sahihi ya idadi yetu hapa nchini
Mrida
0 Comments