KATIBU wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dodoma
Ndg. Jawadu Mohammed ametoa Rai kwa wasimamizi wa Miradi ya Maendeleo
inayotekelezwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kuitunza ili wananchi
wanufaike zaidi na maendeleo yanayoletwa na kiongozi wao Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan katika kila Halmashauri ili idumu
kwa muda mrefu.
Amesema kila mwananchi anapaswa kuwa mwangalifu katika matumizi ya miradi hii kwani huo ndio uzalendo wa nchi kwa kila mtu kujali na kuzingatia miradi inayoletwa kwenye Halmashauri zao.
Ni lazima kuzingatia na kuona umuhimu wa kila mradi unaoletwa na kutumia njia zote kuhakikisha kila huduma muhimu inafika kwenye kila Kata ikiwemo huduma ya maji, umeme, N.k.
Halmashauri ni lazima kuendelea kufanya jitihada za kimaendeleo ili angalau baadhi ya maeneo yenye changamoto zozote za kijamii ziweze kutatuliwa kwa haraka
Ndugu Mohammed.
Vile vile, amesisitiza suala la upandaji miti kwenye mazingira yanayowazunguka ili kuondoa changamoto za majanga kama mafuriko na kusababisha ukame hivyo, kila mwananchi ana jukumu la kupanda miti.
Kwa upande wake, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Dodoma Ndg. Maranyingi Matukuta amesema miradi inakuja kwenye Mkoa wetu ili tuweze kunufaika nayo hivyo miradi hiyo itunzwe vizuri kwani ni miradi yenye thamani nyingi na ni mizuri.
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa Halmashauri inayofanya vizuri kwenye miradi hivo, Rais wetu mpendwa Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ana lengo zuri kwa wananchi wake wa Bahi, hivyo, isimamiwe kwa weledi na watumiaji waitunze
Ndugu Matukuta
Pia ziara ya kamati hiyo iliweza kutembelea Mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Chiona ambayo ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 493, Mradi wa Maji Chali Makulu, Chali Isangha na Chali Igonga inayogharimu kiasi cha Bilioni 2 na kumalizia kwenye Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Chali inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP unaogharimu kiasi cha shilingi Milioni 544.
0 Comments