UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI WA AWALI NA DARASA LA KWANZA UFANYIKE KIKAMILIFU - Mhe. Ndejembi

📌MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhakikisha uandikishaji wa wanafunzi wa awali na darasa la kwanza unaanza kwa kasi na ufanyika kikamilifu.

Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo hayo leo kwa wakurugenzi, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji katika halmashauri hiyo.

Mhe. Ndejembi amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule za msingi na za awali hivyo uandikishaji ni lazima uendane na jitihada zilizofanywa na Mheshimiwa Rais.

Kazi kubwa ya ujenzi na ukarabati wa madarasa katika shule za msingi na awali imefanyika, hivyo watendaji wa Serikali wanapaswa kuhakikisha watoto wote wanaotakiwa kuanza elimu ya awali na msingi wanaandikishwa ili watumie miundombinu iliyongengwa na Rais Samia

Mhe. Ndejembi 

Aidha, Mhe. Ndejembi ametoa wito kwa Halmashauri zote ambazo hazijakamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi na awali pamoja na ambazo hazijakamilisha usajili wa shule kuhakikisha wanakamilisha haraka iwezekanavyo.

Mhe. Ndejembi amesema kuwa, Ofisi ya Rais-TAMISEMI chini ya uongozi wa Waziri Mchengerwa haitomvumilia yeyote atakayebainika kuzembea katika kukamilisha ujenzi wa shule ambazo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi zijengwe kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu.





 

Post a Comment

0 Comments