KAMATI ya siasa ya Mkoa wa Dodoma
ikiongozwa na Katibu Wa Itikadi na uenezi (NEC ) Mkoa wa Dodoma Bw.
Jawadu Mohammed imewapongeza wasimamizi wa miradi inayotekelezwa katika
Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ikiwemo Miradi ya Shule na Hospitali kwa kuzingatia
ubora na ufanisi unaotakiwa.
Akizungumza na baadhi ya viongozi walioshiriki katika ziara ya ukaguzi wa Miradi hiyo Bw. Mohammed amewataka watumishi wa Umma kuitangaza na kuwa Mabalozi Wazuri wa Miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ni lazima tuwe na watu makini wa kufuatilia miradi inayoletwa na Rais wetu ili wananchi wasiwe na changamoto katika kupata huduma na ndio maana zimejengwa shule na Hospitali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri na zinazostahili.
Serikali ipo imara na imedhamiria kuhakikisha wananchi wanapata huduma za umeme, maji, mabweni, madarasa na majengo yote yanakua kwenye ubora na uimara wa Hali ya juu.Ni lazima miundombinu zote zikamilike kwa wakati kama mikataba inavyotaka hatufikirii kuona miradi inavuka muda wake wa utekelezaji
Bw. Mohamed.
Pia Bw. Mohamed amesisitiza suala la upandaji Miti kwa Kila mradi ili kuhakikisha mazingira yanakuwa bora na imara hivyo kudumisha Sera ya Serikali ya Mkoa ya "Kijanisha Dodoma".
Kamati hiyo ilipata fursa ya kutembelea mradi wa Barabara kwa kiwango cha lami uliogharimu Kiasi cha Shilingi Milioni 599, ujenzi wa kituo cha afya Farkwa uliopokea kiasi cha Shilingi Milioni 500, Ujenzi wa Shule ya Msingi na awali Sankwaleto uliopokea kiasi cha shilingi Milioni 396, ujenzi wa Zahanati ya Sankwaleto ambao umepokea kiasi cha Shilingi Milioni 97, na ujenzi wa Mradi wa maji Babayu uliopokea kiasi cha shilingi Milioni 434.
Ukaguzi wa Miradi mbalimbali unaofanywa na Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wa Kamati Bw. Mohhamed ni muendelezo wa ziara ya kikazi wanayoifanya katika halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Dodoma.
|
0 Comments