SIMBACHAWENE AIAGIZA TAKUKURU KUWA NA MAONO UDHIBITI RUSHWA.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuwa na maono ya mbele ya kuhakikisha kunakuwa na mfumo wa kisheria na kiutendaji wa kudhibiti rushwa hasa rushwa ndogo ndogo ambazo zimekuwa kero kwa wananchi.

Simbachawene ameyasema hayo leo Novemba 20 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Taasisi hiyo ambayo amesema rushwa hiyo imekuwa kero kwa wananchi hasa wanapohitaji kupata huduma katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma za elimu, afya ,ofisi za kodi na kwenye utoaji wa leseni.

Aidha Simbachawene amewataka pia kutumia mkutano huo kujadili changamoto zinazowakabili ndani na nje ya taasisi kwa uwazi ili kuweza kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Salum Rashid Hamduni ameeleza mafanikio yaliyopatikana ndani ya mwaka mmoja ikiwemo kuokoa zaidi ya Shilingi Bilioni 171, kupitia operesheni mbalimbali walizozifanya.

Mkutano huo wa siku 3 umebeba kauli mbiu isemayo “Kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu tutimize wajibu wetu” ukiwa na lengo la kujadili utendaji kazi wao kwa kuangalia mafanikio, changamoto walizopata na kuweka mikakati ili kuboresha utendaji wao wa kazi kwa miaka ijayo.



 

Post a Comment

0 Comments