SERIKALI YAWATAKA WAHITIMU KUTUMIA FURSA YA MIKOPO KUPITIA VIKUNDI

 ðŸ“ŒMWANDISHI WETU

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Jenifa Omolo amewataka wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maedeleo Vijijini kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na Serikali kwa kujiunga kwenye vikundi ili kunufaika na mikopo hiyo. 

Omolo ametoa wito huu Novemba 24, 2023 katika mahafali ya 37 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dodoma. Amesema Serikali imezielekeza taasisi za  umma kutoa kazi na ununuzi kwa makundi maalum katika jamii ikiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kwa kiwango kisichopungua asilimia 30. 

Mtaji namba moja ni vijana kujiunga kwenye vikundi. Mtaji namba mbili ni vijana kuwa na nia thabiti ya kufanya kazi kwa kujiunga kwenye kikundi. Itapendekeza sana kama katika vikundi hivi mtwashirikisha vijana wenzenu ambao hawakubahatika kupata elimu ya juu kwa sababu zozote zile

Na hili suala tumekuwa tukiliongelea muda mrefu. Umoja ni nguvu ukitaka kutembea haraka tembea peke yako. Lakini ukitaka kwenda mbali nenda na watu, Kwa hiyo hakikisheni mnajiunga kwenye vikundi

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo hicho Profesa Hozen Mayaya amesema kuwa, chuo kimefanikiwa kuandaa wahitimu wanaoweza kujisimamia wao wenyewe, hivyo wanaamini watakuwa bora katika jamii zao wanazokwenda. 

Wanafunzi wamejengwa kwa mafunzo ya vitendo lakini pia kwa nadharia.

 

Post a Comment

0 Comments