SERIKALI YATOA MIEZI MITATU KWA HALMASHAURI AMBAZO HAZITUMII MFUMO WA NeST


 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

KUFUATIA baadhi ya Halmashauri nchini kutoanza kutumia mfumo wa ununuzi wa Umma (NeST) Serikali imetoa miezi mitatu kwa Wakurugenzi wote ambao hawajaanza kutumia mfumo huo kufanya hivyo.

Aidha takwimu zinaonesha kuwa kati ya Halmashauri zote 184 halmashauri 6 tu sawa na asilimia 3.3 ndizo ambazo zimeanza kutumia mfumo huo.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Sospeter Mtwale ametoa maagizo hayo leo Novemba 23 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Halmashauri ambapo wameandaa mafunzo hayo ili kuweza kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali katika mfumo wa manunuzi.

Mtwale amesema Wakurugenzi wote wanatakiwa kuzingatia sheria na maelekezo yote ya PPRA na kuhakikisha mifumo yote inafanya kazi kwa ufasaha ili kuwahudumia wananchi na kazi ziweze kufanyika kwa wakati.

Watakao kiuka maagizo haya, kwa mujibu wa sheria ya PPRA ni kuwafikisha Mahakamani na kuna faini ya kiasi cha shilingi mil.10 au adhabu ya zaidi ya miaka 3 mpaka 7, kwahiyo semina hii ni kuhakikisha kwamba Wakurugenzi wote wanarudi katika mstari

Amesema kuwa serikali imekuwa ikiboresha mara kwa mara mifumo mbalimbali kulingana na changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza.

Mfumo huo utaenda katika serikali za mitaa na halmashauri zote ambapo katika manunuzi hayo Mkurugenzi afanye manunuzi kwa wakati na kwauwazi

Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Ununuzi wa Umma (PPRA) Eliakim Maswi amesema kuwa hadi kufikia jana halmashauri 69 zimeweza kuwasilisha mipango yao ya ununuzi katika mfumo wa ununuzi,maana yake kuna Halmashauri 115 hazijawasilisha mipango yao ya ununuzi kwenye mifumo yetu ya ununuzi.

Lakini hata hivyo sisi PPRA kwa kushirikiana na Ofisi ya TAMISEMI tuliandaa mafunzo kwa mikoa 26, kwani mikoa yote ilihudhuria na haikuwa na tatizo lolote lile na baada ya mafunzo hayo ya mikoa ambayo PPRA tuliwagharamia tuliomba mikoa ile ikawafundishe halmashauri zetu katika mikoa husika n asisi kama mamlaka tuligharamia ufundishaji ule


 

 

Post a Comment

0 Comments