NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya), Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imeandaa mpango mkakati madhubuti utakaoyawezesha maeneo magumu kufikika kupata huduma za usafiri wa dharura pindi utakapohitajika.
Mhe Dkt. Dugange ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma, wakati alipokua akijibu maswali ya wabunge kwenye kikao cha tatu cha mkutano wa 13 wa Bunge unaoendelea.
Mpango huu umeainisha vyombo vya usafiri vitakavyotumika kusafirisha wagonjwa kwa njia ya anga na maji. Mpango huu unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu na kuanza utekelezaji wake katika mwaka wa fedha 2024/25
Dkt. Dugange
Aidha, Mhe. Dkt. Dugange amesema Ofisi ya Rais-TAMISEMI iliunda timu ya kitaifa ambayo ilichambua na kuandaa mapendekezo ya uendeshaji wa mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri.
Dkt. Dugange ameanisha kuwa, timu hiyo imeshakamilisha jukumu lake na kuwasilisha maoni na mapendekezo ambayo Serikali inaendelea kuyafanyia kazi na mara baada ya kukamilisha zoezi hilo itatoa utaratibu kuhusu mikopo hiyo ya asilimia 10.
0 Comments