MCT YAZINDUA TUZO ZA UMAHIRI WA HABARI TANZANIA (EJAT)


📌SAIDA ISSA

BARAZA la habari Tanzania (MCT) limezindua Tuzo za umahiri wa Uandishi wa habari Tanzania (EJAT) 2023 zenye lengo la kuwaongeza ubunifu waandishi katika kazi zao na kuimarisha taaluma huku likiongeza makundi mapya 2 na kuondoka makundi 3.

Uzinduzi huo umefanyika Jijini Dodoma ambapo waandishi 28 kutoka mikoa tofauti walikuwa wakijengewa uwezo ili waweze kuboresha kazi zao.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya EJAT 2023 Kajubi Mukajanga alisema kuwa tuzo za mwaka huu zitahusisha makundi mawili mapya ambayo ni habari za mifuko ya hifadhi ya jamii na habari za malezi na makuzi ya awali ya mtoto ambayo yameongezwa ili kushajiisha ubora wa uandishi habari katika maeneo hayo.

Pamoja na nyongeza ya makundi hayo makundi ya habari za gesi, mafuta na uchimabaji madini, habari za Sayansi na Teknolojia, na habari za sensa yameondolewa katika orodha ya makundi yatakayoshindaniwa katika tuzo hizo, hii ni kutokana na mwitikio mdogo wa uwasilishaji kazi kutoka kwa waandishi wa habari na kukosekana kwa ufadhili wa uhakika

Amesema kuwa waandishi wenye habari za maeneo hayo ambao wanaona kazi zao ni nzuri wanahimizwa kuziwasilisha kupitia makundi mengine kama uchumi, biashara na fedha au elimu au Kundi la wazi, kutegemea na watakavyoshauriana na wahariri wao.

Ikumbukwe kuwa hii itakuwa ni mara ya 15 kwa kamati ya maandalizi ya EJAT ikiongozwa na MCT kuandaa mashindano hayo mfululizo bila kukosa ambapo kwa mara ya kwanza yalifanyika 2009 tuzo hizo zililenga kuwatambua na kuwatunza waandishi wa habari walifanya kazi zao vizuri katika makundi mbalimbali ya kushindaniwa katika mwaka husika.

Kwa upande Mkurugenzi wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya amesema kuwa ni muhimu sana kuandika habari za malezi ya awali kwa watoto ni kitu muhimu ambacho waandishi hawajakupa kipaumbele.

Kwa kuingizwa kwenye tuzo za EJAT maana yake tunataka kuona mnaanza kujikita katika masuala haya kwani masuala haya yana faida kubwa sana kwa Nchi, hasa kwa kuzingatia kwamba mtoto inatakiwa aanze kujengewa uwezo kuanzia miaka 0 na hii itasaidia sana endapo mtoto atalelewa katika mazingira mazuri

Licha ya kamati ya maandalizi ya EJAT kutoa tuzo na zawadi kwa washindi pia MCT hutoa udhamini wa masomo wenye thamani ya shilingi za kitanzania Milioni 3 kwa mshindi wa jumla ili ajiendeleze kitaaluma katika masuala ya uandishi wa habari kulingana na mahitaji yake.

Katika mashindano ya mwaka huu EJAT, MCT itaendelea na tuzo ya mshindi wa maisha katika uandishi wa habari (LAJA) ambayo itakuwa ikitolewa kwa mara ya nne, tuzo hiyo hutolewa mwandishi aliyetoa mchango mkubwa katika kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari na uhuru wa vyombo vya habari.

Tamasha la EJAT 2023 limepangwa kufanyika Julai 27,2024 hivyo mwisho wa kuwsilisha kazi za waandishi ni Januari 31, 2024 ambapo utaratibu wa kuwsilisha kazi utakuwa wa aina mbili Kwa njia ya Mitandao (online form) au kwa kuwasilisha fomu ambayo inapatikana kwenye tovuti ya MCT ya www.mct.or.tz




 

Post a Comment

0 Comments