SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson leo Novemba 6, 2023 bungeni jijini Dodoma amesema walimu wawili waliovuliwa madaraja Wilayani Tunduma Mkoani Songwe kwa kosa la kucheza muziki wa bongo fleva na wanafunzi warudishwe katika nafasi zao kwa kuwa mamlaka husika haikutoa nafasi ya pande mbili kuwasikiliza walimu hao.
Katika hali ya kawaida hata sisi waheshimiwa wabunge huwa tunacheza mziki na wanafunzi na isitoshe hata walimu wakuu wenyewe wanakili hawakuwepo shuleni mamlaka iwarejeshe katika nyadhifa zao kwa kuwa hawakusilizwa au mnachukua hatua bila kuwasikiliza?
Dkt.Tulia
Hayo yamejiri kufuatia Mbunge wa Viti Maalum wa CCM Mhe Husna Sekiboko kutoa hoja kuhusu nyimbo za muziki kupigwa kwenye taasisi za elimu kwa maana ya shule za msingi na sekondari na hatua ambazo zinazoweza kuchukulia kufuatia jambo hilo huku akisema Serikali itoe kauli nyimbo zipi zinaruhusiwa na zipi haziruhusiwi.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kuhusu suala la maadili shuleni na suala la muziki inayopigwa shuleni na hatua ambazo serikali inaweza kuchukua amesema wanalo jukumu la kusimamia malezi shuleni kudhibiti aina ya muziki inayoruhusiwa shuleni na kukataza ambayo inakiuka maadili ya kitanzania.
Amesema Waraka wa mwisho wa kamishina wa elimu ulisisitiza hata kwenye mabasi ya shule kuzingatia baadhi ya nyimbo hizo huku akisema siyo kila kitu kinachokubaliwa uraiani kinakubaliwa shuleni.
Kadhalika amesema walimu hao kama hawataridhishwa na hatua hiyo ya kinidhamu wanayo nafasi ya kukata rufaa
0 Comments