KITUO CHA FORODHA KUJENGWA KAKOZI, MOMBA.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

NAIBU Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande amesema Serikali inakwenda kujenga kituo cha Forodha Kakozi wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Momba, Mhe. Condester Sichalwe, aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali wa kuweka Kituo cha Forodha, eneo la Kikosi, Wilaya ya Momba, ili kuunga mkono jitihada za kujenga Soko la Mazao la Kimataifa.

Chande amesema kuwa, Serikali kupitia TRA ina utaratibu wa kupitia na kufanya tathmini sehemu zote zinazoweza kujengwa Ofisi kwa ajili ya ukusanyaji kodi, utaratibu unazingatia uwiano wa gharama za ukusanyaji wa mapato na kiwango cha kodi kinachotarajiwa kukusanywa

Serikali inaendelea kufanya tathmini ya kina katika maeneo mengi ikiwemo Kakozi, Wilayani Momba. Maeneo yatakayokidhi vigezo vya kujenga Ofisi za Forodha, taratibu za uanzishwaji wa Ofisi zitaanza kwa kuzingatia upatikanaji wa rasilimali watu na fedha

Mhe. Chande.

Aidha, Mhe. Chande alisema kuwa tathmini hiyo itakamilika ndani ya mwaka wa fedha 2023-2024. 

Namuelekeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aangalie uharaka wa ujenzi wa Kituo cha Forodha-Kakozi, Wilaya ya Momba endapo atajiridhisha kutokana na tathmini yake

Mhe. Chande.

 

Post a Comment

0 Comments