📌RHODA SIMBA
IMEELEZWA kuwa, takriban kina mama milioni mbili hapa nchini hujifungua, ambapo kati ya hao laki 220,000 hupata watoto waliozaliwa chini ya wakati ambayo ni sawa na asilimia 11.
Pia, zaidi ya watoto 50,000 wenye umri wa chini ya siku 28 hufariki, ambapo watoto 13,500 sawa na asilimia 27 ya vifo hivyo hutokana watoto kuzaliwa kabla ya wakati.
Hayo yameelezwa leo na Mkurungenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ikiwa ni maadhimisho ya siku ya watoto njiti ambayo huadhimishwa kila ifikapo Novemba 17 ya kila mwaka.
Dkt. Chandika amesema Hospitali ya Benjamin Mkapa imeendelea kutoa huduma kwa watoto wachanga wakiwemo watoto waliozaliwa kabla ya wakati, ambapo inaelezwa kuwa idadi hiyo imeendelea kuongezeka mwaka 2021 ambapo walihudumia watoto 25 waliozaliwa kabla ya wakati.
Maadhimisho ya sikuku hiyo yanaenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Vitendo Vidogo, Matokeo Makubwa”
0 Comments