WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, mipango na
uwekezaji amesema kuwa katika eneo la Tanganyika Packers Mbalizi (Shamba Na.761
la kulishia mifugo la Nsalala lenye Ukubwa ekari 4,900), Serikali imefanya
maamuzi ya kulikabidhi eneo hilo kwa Mamlaka ya Maeneo Maalum kwa Mauzo Nje
(EPZA) kwa ajili ya Uwekezaji.
Hayo ameyaeleza Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza alipouliza kuwa Je, kuna Mkakati gani wa Kujenga Viwanda Maalum na Maghala ya ubaridi kwenye eneo la Tanganyika Packers Mbalizi?
Waziri amesema kuwa Baada ya makabidhiano, eneo hilo litatumika kwa ajili ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Viwanda mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, Serikali imechukua maoni ya Mheshimiwa Mbunge ya ujenzi wa viwanda maalum na maghala ya ubaridi katika eneo hilo na itayafanyia kazi
0 Comments