📌MWANDISHI WETU
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi ACP Kaster Ngonyani amesema hakuna kamata kamata tena kwa waandishi wa habari, waandishi wa habari ni ndugu zetu, ni sehemu ya jeshi letu tuwalinde.
Ameyasema hayo wakati akichangia mada katika Mdahalo kuhusu Ulinzi na Usalama kwa mwandishi wa habari ulioandaliwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Katavi ambapo ameongeza kuwa jeshi la polisi limefanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji hivyo hakutakuwa na ukamataji wa Waandishi wa habari usiofuata sheria kama ilivyokuwa siku za nyuma
Aidha ameongeza kuwa uandishi wa habari sio vita hivyo ni muhimu jeshi la polisi kuwaheshimu waandishi wa habari vilevile waandishi wa habari kuwaheshimu jeshi la polisi.
Hata hivyo, ACP Ngonyani, ameahidi kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari na kusisitiza kuwa madhila yaliyowapata Waandishi wa habari wakiwa kazini huenda yalisababishwa na ukiukaji wa maadili kwa askari waliohusika katika matukio hayo
Naye SSP. Juma A. Jumanne amewataka Waandishi wa habari kuacha vitisho dhidi ya polisi ili kuimarisha mahusiano baina ya pande zote mbili.
Tukiacha vitisho na victimization (kutuhumu) mahusiano na jeshi la polisi yataimarika
SSP. Jumanne
Mdahalo huo umefanyika jana tarehe 16.11.2023 katika ukumbi wa St. Matiasi Mpanda Mjini.
0 Comments