SERIKALI
imesema kuwa katazo la matumizi ya kuni na mkaa litazihusu tu taasisi zote za umma
na zabinafsi na si kwa mwananchi mmojammoja kama inavyotafsiriwa.
Imesema
Taasisi zote za Umma na Binafsi Tanzania Bara zinazoandaa chakula na kulisha watu
zaidi ya 100 kwa siku kusitisha matumizi ya kuni na mkaa ifikapo Januari 31,
2024 wakati zile zinazoandaa chakula na kulisha watu zaidi ya 300 kwa siku zinapaswa
kusitisha matumizi ya nishati hiyo ifikapo Januari 31, 2025.
Akitoa
ufafanuzi huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mhe. Dkt. Selemani Jafo lengo la Serikali ni kudhibiti uharibifu wa mazingira kutokana
na ukataji miti kwa kiwango kikubwa na kulinda afya za wananchi.
Bahati mbaya sana baadhi ya watu walitafsiri lile tangazo tulilotoa mwezi wa nne wakawa na wasiwasi kuwa sasa itakuwaje hata mama ntilie au majumbani watashindwa kupika, hapana si hivyo lengo letu ni kuanza kwa taasisi zenye watu wengi.
Ni kweli shule zetu ni watumiaji wakubwa wa kuni, nenda katika taasisi zetu zingine utaona namna gani kuni zinatumika ndio maana tukatoa maagizo haya kwetu sisi wenyewe (taasisi za Serikali na taasisi binafsi) kwanza tuanze kujipanga katika hili na tutasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira
Dkt. Jafo.
Amesema
kuwa matumizi ya kuni na mkaa yanaathiri afya ya mtumiaji kwa kusababisha magonjwa
yatokanayo na kuvuta hewa chafu ambayo huathiri mapafu, moyo na matumizi ya muda
mrefu wa nishati hiyo pia husababisha magonjwa ya macho.
Kwa
mujibu wa Ripoti ya Tatu ya Hali ya Mazingira nchini ya mwaka 2019 kasi ya uharibifu
wa misitu ni kubwa na kila mwaka zaidi ya hekta 469,420 huharibiwa kutokana na
ukataji wa miti kwaajili ya matumizi ya kuni na mkaa.
Halikadhalika
inakadiriwa kuwa asilimia 16 ya ardhi imeharibika na inakabiliwa na kuenea kwa hali
ya jangwa na ukame kutokana na watu wengi kufanya shughuli zisizo endelevu ikiwemo
kutumia nishati ya kuni na mkaa kwaajili ya kupikia kutokana na nishati hiyo kupatikana
kwa urahisi na watu wengi wanaweza kumudu gharama yake.
Hivyo,
kutokana na athari hizo zilizojitokeza, kipaumbele cha Serikali kwasasa ni kujenga
uchumi wa viwanda, matumizi ya nishati mbadala ikiwemo mkaa mbadala yatatoa fursa
ya viwanda vya kutengeneza mkaa mbadala sanjari na kuzalisha majiko sanifu na
banifu kwaajili ya matumizi fanisi ya nishati hiyo.
Waziri
Jafo ametoa wito kwa kampuni za gesi, mkaa mbadala na majiko banifu zitumie katazo
hili kama fursa ya uzalishaji wa bidhaa hizo kwawingi kwaajili ya kupanua wigo wa
masoko kwa taasisi hizo.
Itakumbukwa
kuwa Juni Mosi 2021, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa alitoa tamko la Wiki ya Mazingira Duniani na kuzielekeza Taasisi,
Mashirika ya Serikali na Sekta Binafsi zianze kutumia nishati mbadala kwa kupikia
na shughuli nyingine za uzalishaji.
1 Comments
..Tuzidi kuhabarika na kuelewa mwelekeo wa Serikali katika kumpa Mwananchi maendeleo. 🤔🤔
ReplyDelete