TAASISI za ujenzi zimekiri moja ya changamoto wanayokutana nayo ni upandaji wa bei za vifaa vya ujenzi hivyo wameiomba Serikali kuliangalia jambo hilo kwa umakini.
Hayo yameelezwa na Meneja wa kampuni ya mradi wa nyumba na viwanja Iyumbu-Dodoma Venny Construction &Real Estate Co.Ltd Mussa Mwambalile kwenye maonyesho ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali jijini Hapa ambapo maonyesho hayo yalianza Oktoba 3, 2023 na kufikia kilele Oktoba 5
Amesema kuwa changamoto wanayokutana nayo ni upandaji wa bidhaa za Ujenzi hivyo kupelekea ugumu katika shughuli zao hivyo kujikuta wakipata maswali mengi kwa wateja wanao wajengea nyumba.
Wateja wetu waelewe zinapopanda gharama za vifaa vya ujenzi nasisi gharama za nyumba zinaongezeka kwahiyo tunakutana na wakati mgumu kumuelewesha mteja kwamba gharama za Ujenzi wa nyumba zipo juu kutokana na upandaji wa vifaa vya ujenzi mfano kwenye simenti, bati na vifaa vingine vya ujenzi
Aidha Meneja huyo amesema kuwa kutokana na Dodoma kuwa makao makuu ya nchi ujio wa watu wengi wanaohitaji nyumba umekuwa mkubwa hivyo kampuni hiyo itahakikisha inaendelea kujenga nyumba za kisasa na bora kwaajili ya mahitaji yao.
Kuhamishiwa kwa Wizara na Taasisi za Serikali imekuwa chachu kwetu sisi kupata wateja na biashara yetu kuwa nzuri hivyo tunaiahidi Serikali ya awamu ya 6 kuendelea kushirikiana nayo kwa karibu kuhakikisha watumishi na watanzania wanapata makazi Bora
Aidha amesema kuwa kampuni ya Venny itaendela kujenga nyumba zenye ubora huku kipaumbele kikiwa ni utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti katika nyumba hizo ili wateja wao waweze kuwa na mazingira rafiki.
Pia ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma kuitumia kampuni hiyo katika ushauri wowote unaohusiana na masuala ya Ujenzi kupata ushauri wa kitaalamu katika kampuni hiyo.
0 Comments